Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,310
- 4,538
USITUFUNGE MDOMO.
1)Mikono ina sauti,kali kuliko ya radi.
Ulipuka kwa kishindo,inapopanda midadi.
Acha mdomo useme,hata kama siyo jadi.
Usitufunge midomo,mikono itaongea.
2)Busara hata hekima,ndo vazi la babu zako.
Ubabe uso na kimo,isiwe tabia yako.
Endelea utaona,yalowakuta wenzako.
Usitufunge midomo,mikono itaongea.
3)Tazama mfano huu,wa nahodha mfa maji
Abiria huwa tisha,akijua mjuaji.
Mwisho wa tembo ni ndovu,hufa kama bata maji.
Usitufunge midomo,mikono itaongea.
4)hili pango la ajabu,wewe uliingiaje.
Najua chanzo ni sisi,hivi leo wakuaje.
Sasa tutakaa kimya,twasubiri muda uje.
Usitufunge midomo,mikono itaongea.
5)Hakuna atosimama,wote watakukimbia
Damu ndo itanukia,hilo sitokuombea.
Dalili zinaonyesha,kile wakiangamiza.
Usitufunge midomo,mikono itaongea.
6)Mwisho wa sumu kuinywa,hiyo unayoimeza.
Unapandikiza chuki,vibaya nakueleza.
Usitutie uwoga,mchezo tutaucheza.
Usifunge midomo,mikono itaongea.
7)Babu hafunzwi hadithi,na mjukuu wa jana.
Kama bado ni kipofu,basi wabane vijana.
Mori ukisha wapanda,akili zitawabana.
Usitufunge midomo,mikono itaongea.
Shairi=USITUFUNGE MDOMO.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninha@gmail.com
1)Mikono ina sauti,kali kuliko ya radi.
Ulipuka kwa kishindo,inapopanda midadi.
Acha mdomo useme,hata kama siyo jadi.
Usitufunge midomo,mikono itaongea.
2)Busara hata hekima,ndo vazi la babu zako.
Ubabe uso na kimo,isiwe tabia yako.
Endelea utaona,yalowakuta wenzako.
Usitufunge midomo,mikono itaongea.
3)Tazama mfano huu,wa nahodha mfa maji
Abiria huwa tisha,akijua mjuaji.
Mwisho wa tembo ni ndovu,hufa kama bata maji.
Usitufunge midomo,mikono itaongea.
4)hili pango la ajabu,wewe uliingiaje.
Najua chanzo ni sisi,hivi leo wakuaje.
Sasa tutakaa kimya,twasubiri muda uje.
Usitufunge midomo,mikono itaongea.
5)Hakuna atosimama,wote watakukimbia
Damu ndo itanukia,hilo sitokuombea.
Dalili zinaonyesha,kile wakiangamiza.
Usitufunge midomo,mikono itaongea.
6)Mwisho wa sumu kuinywa,hiyo unayoimeza.
Unapandikiza chuki,vibaya nakueleza.
Usitutie uwoga,mchezo tutaucheza.
Usifunge midomo,mikono itaongea.
7)Babu hafunzwi hadithi,na mjukuu wa jana.
Kama bado ni kipofu,basi wabane vijana.
Mori ukisha wapanda,akili zitawabana.
Usitufunge midomo,mikono itaongea.
Shairi=USITUFUNGE MDOMO.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninha@gmail.com