Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 1,118
- 1,565
Yer 11:10 SUV
[10] Wameyarudia maovu ya baba zao, waliokataa kusikia maneno yangu; wamewafuata miungu mingine na kuwatumikia; nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda, wameyavunja maagano yangu niliyoyafanya na baba zao.
Kinachoonekana hapa katika andiko hili, yapo mambo kadhaa ila ninataka tukijite zaidi kwenye kurudia maovu ya baba zao, au yale maovu waliyoyaacha huko nyuma.
Hapa inaonyesha kuwa kulitokea mzunguko wa dhambi katika kizazi hichi, uliokuwa unarudiwa kizazi kimoja na kingine. Mambo mabaya yaliyotendwa na kizazi hichi, yalitendwa na kizazi kingine.
Tunaweza kusema kuwa kulikuwa na dhambi za mzunguko au za kurithi kama wengine wanavyofundisha au kuhubiri siku za leo kuwa kuna laana za ukoo anazo mtu, jambo ambalo sio sahihi kwa mtu aliyemwamini Yesu Kristo. Sasa hapa haikumaanisha walikuwa wanarithi dhambi kiroho, walikuwa wanaiga mienendo ya mababu zao waliyokuwa wanatembea nayo bila kutubu.
Hapa tunapata elimu kubwa kuwa tunapaswa kutubu kweli na kupokea mabadiliko mapya kiroho, kuyaacha kabisa yale maisha ya zamani ya dhambi na kutoyarudia tena.
Huu ni uamuzi wa mtu binafsi, anapaswa kuufanya anapotaka kujenga uhusiano mpya na Mungu wake, yale maisha ya dhambi anapaswa kukaa nayo mbali kweli, na sio kuendelea nayo au kuyarudia mabaya baada ya kukaa nayo mbali muda fulani.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana