Usioe mwanamke masikini

David Harvey

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2014
Posts
3,119
Reaction score
6,785
Habarini wapendwa?

Miaka mitatu iliyopita nilileta thread ikisema "usioe mwanamke masikini"
Baada miezi 3 kuoa ndugu wa mwanamke walihamia nyumbani kwangu kutoka kijijini kwao walikuwa 11 wakiume walikuwa 7 wakike 4.

Kiukweli nilikwazika sana na ujio wao ukiangalia dar maisha ni tough kibaya zaidi walikuwa wanakula mno kama fundukwi mpka nikaja jf kuomba ushauri.

Ila kuna wadogo wawili wa mke wangu nilihamua kujitolea kuwasomesha nilikuwa nawaonea huruma sana..

Ila niwaombe radhi sana mashemeji zangu niliwakosea sana nilikuwa nawatukana sana moyoni ila leo hii mmekuwa baraka kwangu mmekuwa msaada mkubwa sana kwangu.

Nina miaka miwili tangu nifukuzwe kazi ila hawa mashemeji niliowachukia leo hii ndio wanaonipiga tafu wanasomesha watoto wangu 3.wawili wapo marian girls na mmoja yupo anasoma tusiime nadhani wote mnajua ada na gharama ya hizo shule

Lakini leo hii wale niliowasaidia kwa chuki pasipo wao kujua kama nawachukia leo ndio wanao nisaidia na wana pesa c mchezo ingalikuwa hawajasoma.Wale mashemeji wadogo niliowasomesha hivi sasa wapo muhas mwaka 3.

NB: Usichukie masikini wasaidie kama una uwezo waheshimu ndugu wa mke wako maana haujui kesho yako. Nisameheni wote niliowakwaza kwa ile thread yangu miaka 3 iliyopita.

Jumapili njema
 
Me sijaelewa, kwann umesema usioe mke masikini halafu chini ulichozungumzia na ushauri uliotoa vinakinzana na jina la uzi?!

Aisee unajua ifike wakati muwe mnaangalia mnavyopost sio kupost uzi na vitu vya kutunga tunga wengine humu ndani ni watu wazima na tupo hapa kuwashauri nyie akina bwana mdogo ambao siku hizi bila ushauri mnapotea sana
 
Hadithi inatufundisha; " Usioe mwanamke maskini, mashemeji watakuja kukupiga tafu"
 

Miaka mitatu tu iliyopita mambo yote hayo yametokea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…