Usimeze matunda, uwe unatafuna

Usimeze matunda, uwe unatafuna

Bwana Matunda

New Member
Joined
Jul 16, 2021
Posts
4
Reaction score
5
"Ili mtu uweze kupata faida(virutubisho) kutoka kwenye chakula ni lazima chakula iko kipite katika mfumo wa umeng'enywaji chakula(digestive system) ambao unatumia organ zake mbalimbali ili kumeng'enya chakula na kufyonza virutubisho katika chakula.

Mdomo(mouth) ndio organ ya kwanza inayotumika katika umeng'enyaji wa chakula. Katika mdomo kuna kimeng'enyaji chakula(mate). Katika mdomo kazi kuu ni kuvunjwa vunja vyakula kundi la carbohydrates (wanga) na aina nyingine ya vyakula.

Kitendo cha kuvunja vunja chakula kinaitwa KUTAFUNA(chewing).
Kwa maana iyo bila kutafuna chakula vizuri viungo vingine vilivyo katika mfumo wa umeng'anyaji chakula ushindwa kufanya kazi kwa ufasaha,maana kila organ ina kazi yake katika mfumo wa chakula.

USHAURI WANGU
Matunda ni moja ya chakula kilicho sheheni virutubisho mbalimbali kama carbohydrates, mafuta,protini,vitamini,madini n.k.

Ivyo katika ulaji wa tunda lolote unalokula hakikisha unatafuna vizuri.

Tusiwe tunakula matunda bila kutafuna,sababututakuwa tunakosa virutubisho vilivyo katika hayo matunda. Kwa wale wanao meza tu bila kutafuna (chewing) tuache tabia iyo na tuanze kutafuta tena taratibu na kwa uhakika.

Utafunaji katika mdomo utumia meno,msiniulizewasio na meno watatafuna vipi hayo matunda.

Ndimi Bwana Matunda
 
Mfano tunda la strawberries je unaweza kutafuna
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom