USILOLIJUA LITAKUSUMBUA
By
Charles Mwijage
Waziri wa viwanda
Taifa letu linapambana kuingia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 au kabla ya hapo. Hayo yako kwenye dira ya taifa 2025, Ilani ya CCM 2015-20, mpango wa pili wa miaka mitano 2016/21 na hotuba za Mh Rais Magufuli kwa vipindi tofauti.
Mambo muhimu:
- Tunajenga uchumi wa viwanda tukilenga kuchochea mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu.
-Huu ni uchumi jumuishi ambao maendeleo ya vitu yataenda sambamba na maendeleo ya watu.
-Wananchi kwa wingi wetu wataunganishwa katika mnyororo wa kuongeza thamani au uzalishaji wa bidhaa au utoaji wa huduma.
- Njia ya haraka ni hii tuliyochagua, uchumi wa viwanda. Tanzania sasa tunajenga viwanda.
- Wananchi wameelewa somo kuliko dhima yoyote kabla ya hapo na hamu ya wananchi ni kubwa.
-Hotuba ya Wizara ya viwanda ambayo hiko kwenye Website yetu, viwanda vyenye thamani ya trillion 5.25 vimeanzishwa vikiwa hatua mbalimbali za ujenzi.
- Vifaa vya ujenzi ikiwemo saruji , vigae, nondo na mabati sasa tunatosheleza mahitaji na tunauza nje. Hili ni kundi la vifaa vinavyotumika sana.
- Viwanda vya matunda, maji, maziwa, nyanya vimeanzishwa tukilenga kujenga soko la mazao ya wakulima ndani na nje ya nje. Mh Rais tayari amezindua kiwanda cha kukausha matunda asilia mahsusi kwa soko la Ulaya na Kiwanda kinadai malighafi. Punde Sayona watakamilisha Kiwanda kinachochakata tani 300 za matunda kwa simu (truck trailers 10) pale Msoga na kiwanda cha vinywaji Mwanza kinasubiri uzinduzi
- Tumeanza uwekezaji wa sukari. Mkoa wa Morogoro tu tutazalisha tani takribani laki 5. Mkulazi tani laki 2.5, Mbigiri tani laki 0.3, Moro Sugar laki 1, Mtibwa itaongeza laki 1. Orodha ya miradi mipya.
- Viwanda vilivyokufa kwa Agizo la Mheshimiwa Rais vimeanza kufufuka. Dabaga wamefunga mitambo mipya nafungua September, Moproco ukarabati wa mitambo unekamilika wanasubiri leseni ya export, Bora wameanza kuzalisha viatu, DOWICO Dodoma imerudi ya kisasa zaidi, Manonga Ginnery na Tabora Nyuzi inakarabatiwa
- Wamiliki niliwambia waje niwaelekeze namna ya kufufua viwanda, wameanza kuja kweli. Na sawa ni moja tu, PIMS - yaani kama huwezi mwalike nwingine ushirikiane naye upate angalau stahili yako.
- Tunataka viwanda vifanye kazi ili tupate ajira- asilimia 65 ya Watanzania ni vijana wenye umri usiozidi miaka 35. Asiye wahurumia vijana wasio na ajira atuache sisi tulioahidi.
- Viwanda vifanye kazi tupate bidhaa kwa matumizi yetu na mauzo nje kupata fedha za kigeni
- Viwanda vifanye kazi tuongeze wigo wa walipa kodi wa uhakika ili tupate fedha za kuleta maendeleo ya watu.
Tanzania sasa tunajenga Viwanda
*Charles Mwijage*
*Nimetumwa viwanda - Hanoi Vietnam*
Sent using
Jamii Forums mobile app