Usikurupuke kwenye biashara

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
75,227
157,421
KUKURUPUKA NI SUMU KWENYE BIASHARA.
Ni kweli kabisa mtaji unao, na shauku unayo na mpango unao bado usikurupuke.
Mara nyingi sehemu kubwa ya watu wenye nia njema wanashindwa kutekeleza nia zao na makusudi yao kwa sababu ya kukurupuka.
Wengi wamekurupuka na kujikuta katikati ya mteremko wa kuanguka kiuchumi baada ya kuanzisha biashara kwa mihemko pasipo kufanya analysis ya kutosha.
Mtafiti mmoja alisema kati ya makampuni 100 yanayoanzishwa marekani ni makampuni 8 tu yanafanikiwa kufika kweye top ya mafanikio.
Makampuni tunayoyasikia leo ikiwemo Dell, Apple, Ford nk ni miongoni mwa baadhi ya makampuni machache yaliyofanikiwa kati ya makampuni mengi yaliyofia njiani.
Biashara unayoiona leo au ya mtu fulani inawezekana hailipi au hata yeye anatamani kuiacha au anaifanya kwa sababu hana cha kufanya ila tatizo ni mara chache watu wanakuwa wazi kukwambia ukweli ila wengi wenye biashara pamoja na mengi wanayojua kuhusu biashara zao huwa hawasemi ukweli watakueleza inalipa ila mimi sina hiki na hiki ila kingekuwepo ingelipa.
Mara nyingine usione tu mtu anafanya biashara pengine ana namna fulani inafanikiwa na hawezi kukueleza jinsi anavyofanya kwa sababu mbali mbali ikiwemo uhalifu, wewe unapokurupuka na kuanzisha biashara kama hiyo kwa vyovyote utaanguka maana kuna njia za siri hauzifahamu.
Kabla ya kuanzisha biashara yeyote pata muda wa kufuatilia kwa makini na kwa undani aina ya biashara unayotaka kuanzisha.
Jifunze kuwa na sababu binafsi za kuanzisha hiyo biashara sio kisa mjomba ameifanya na mimi nafanya.
Kuwa na plan B ikiwa utakutana na changamoto katika hiyo biashara utafanya nini ?
Usiingize mtaji wako wote unapoanza hiyo biashara, pima kina cha maji kwanza kabla hujadumbukiza miguu yote.
Usikurupuke tuliza akili yako kwanza........
Jiulize katika maisha yako utaanzisha biashara mpya mpaka lini ?
Kwanini usianzishe biashara moja ukaifanya miaka 20 uone kama haitakufikisha mbali ?
Simamia maamuzi yako baada ya kuamua aina gani ya biashara uifanye , bila hivyo utachukuliwa na kila upepo.
Uwe na Mwanzo mwema wa biashara yako ......
©Charles Cosmas
0762287224
 
Kwa luongezea biashara nyingi huchafua mazingira....
 
Back
Top Bottom