Usikate tamaa!

Usikate tamaa!

kwamtoro

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2010
Posts
4,922
Reaction score
3,244
Kwa muda mrefu nimegundua hamna mstari wa mwisho kwa kila moja katika mbio za kimaisha

Usafiri wetu ni tofauti na muda wetu ni tofauti. Kwa mfano, mtu moja anamaliza chuo akiwa na umri wa miaka 20 na kisha anahangaika kutafuta kazi anapata kazi akiwa na miaka 25. Na mwingine anamaliza chuo akiwa anamiaka 25 kisha ndani ya muda mfupi anapata kazi akiwa na miaka hiyo hiyo 25.

Mwanaume anamuoa msichana bikra na anasubiri kwa muda mrefu ndipo anapata watoto. Na msichana mwingine anakuwa ametoa mimba nyingi tu katika maisha yake kisha ndani ya muda mfupi tu baada ya kuolewa anapata watoto.

Mtu anakuwa mkurugenzi akiwa na miaka 38 kisha anakufaa akiwa na miaka 56. Mwingine anakuwa mkurugenzi akiwa na miaka 55 kisha anakufa akiwa na miaka 90.

Ni maisha! Maisha ni upepo mwingi, unabadilika, juu na chini na mishangao mingi na mahudhuniko mingi.
.
Maisha yanampa kila mtu na kila moja kati yetu bahati mbalimbali, na kipindi bahati ikipotea, inaondoka kimoja ikitokea tena labda ni kwa neema ya Mungu. Ni jukumu la kila moja wetu kuwa tayari, kusubiri, kutambua na kutumia kila bahati katika maisha yake. Tunajifunza katika safari. Hamna kati yetu ambaye anavyo kila kitu au anafahamu kilakitu. Na ndio sababu ya kuto anguka wote kwa wakati moja.


Na ndio maana kama moja yupo chini, hajiwezi, amekata tama, wengine ambao wapo imara wanampa moyo na kumnyajua juu mwenzao. Tunafahamu maisha ni magumu, tujifunze kwenda tukimtegemea Mungu na pengine hata onyesha njia sasa ila atakuonyesha njia siku nyingine. Katika kila ukijaribu, unapata ugumu au mda mwingine una anguka, yote yatapita. Tutanyanyuka, tutakuwa wenye nguvu tena na kuwanyanyuwa walio chini. USIKATE TAMAA.
 
mkuu wewe ni mtafiti..........................loading error......................
 
mkuu nimeipenda hii
Mtu anakuwa mkurugenzi akiwa na miaka 38 kisha anakufaa akiwa na miaka 56. Mwingine anakuwa mkurugenzi akiwa na miaka 55 kisha anakufa akiwa na miaka 90
 
Ujembe mzuri sana unatia moyo.
 
Duuuuh! ubarikiwe sana asee yaan umenitia moyo sana nmejkuta nmepeta nguvu ghafla.
 
Back
Top Bottom