Usikatae mzungu ni genius

aduwilly

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2009
Posts
1,191
Reaction score
320
Mzungu ni genius jamani, wala msibishe, unachukua mamilioni Afrika wewe mwenyewe unaenda yaweka kwa Mzungu, kisha Mzungu anayachukua anakuja kukukopesha kwa riba kubwa hadi deni la Taifa linafikia trilioni 52.

Pesa yako mwenyewe kisha unakopeshwa halafu unamtukana mtu anaekwambia mzungu ni genius. Tena Mzungu mmoja aliwaambie waafrika mkitaka niwasaidie fedha (ambazo ni zenu mmeziweka kwake) kuweni mashoga sivyo misaada kiduchu. Wengine wanakubali (Malawi) wengine wanajidai bado wapo wapo kwanza.

Usikatae mzungu ni genius
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…