Usijaribu utapeli huu wa kuambiwa utapata pesa za kiurahisi mtandaoni

D Metakelfin

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
3,193
3,325
TAHADHARI! UKWELI KUHUSU WIZI WA MITANDAO YA REVENUE BRUST, ONLINE TASK PAY, YOUTHNIZER N.K.

Your Payment Withdrawal
Option will appear here, when you will reach you minimum payout limit of 300$
You need [ 275 $ ] to get payout request form.

Baada ya kupigiwa simu na watu mbalimbali wakihitaji kujua uhakika wa pesa inayotangazwa kwenye mitandao ya OnlineTaskyPay, Money4Task.

Anatory enterprises tumetafuta ukweli kuhusu hili. Kama ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii utakuwa tayari umeshakutana na post hasa kwenye mitandao ya WhatsApp inayokutaka ubonyeze link fulani ili ujipatie hela. Unapojisajili tu unapewa Dola 25 mitandao mingine unapata dola 10 na kadhalika ambayo kwa Tanzania ni takribani Elfu 60 kitu ambacho watu wengi wamekuwa wakijiingiza huko bila hata kujua hatma yake.

Kwa uhakika mitandao hiyo ni ya uongo na ya kitapeli. Malengo ya mitandao ya namna hiyo ni kukupotezea muda, kuwatangaza wafahamike kwa kuwa traffic wanaoyipata kupitia link hizo huhamishwa kwenda kwenye tovuti ambazo baadae wanazifunua na hatimaye kukuibia taarifa zako kama za anuani, barua pepe yaani e-mail na taarifa nyinginezo za kisiri.

Kwanini mitandao hii ni ya uongo na kitapeli?

1. Hakuna usalama wa kutosha kwa mtumiaji,mtu unajisajili kwa dakika 1 na taarifa zako ni email, username na jina la hundi (Cheque), kitu ambacho hakiwezekani kwa miamala ya kifedha.

2. Mtandao unohusika huwa ni mmoja tu ambao huwa unatumia majina tofauti tofauti mfano mwanzoni ulianza na jina la OnlineTaskPay ,baadae ukabadilishwa na kuwa Money4Task na sasa unajulikana kama Youthnize. Lakini umeibuka tena mwingine unaoitwa Revenuebrast.

3. Ukishafikisha $300 au mingine mitandao wanataka dola 400 n.k. na kuendelea utahitajika uthibitishe kama wewe siyo roboti kwa kubonyeza link fulani ambapo link hiyo haifunguki kamwe.

4. Malipo yote wanayatangaza kuwa hutolewa kuanzia tarehe 24-30 na usipofungua akaunti yako kwa siku 30 akaunti yako inafungwa . Muda huo wa malipo ukifika huwa wanabadilisha jina kama ambavyo nimeeleza hapo juu.

5. Muundo wa Mtandao yaani Dashboard au Homepage ina taarifa za aina moja na ndiyo ushahidi wakusema kuwa mtandao huo ni mmoja ambao unabadilishwa jina tu. Japo muonekano wa mtandao wa sasa umebadilishwa kuliko ya zamani iliyotangulia.

6. Baadhi ya mitadao hiyo haina anuani ya ofisi zao yaani Physical Address kitu ambacho tumekizoea kwa matapeli wa mitandaoni. Ukurasa wa OnlineTaskPay. Baada ya kufikia mwezi wa 9 kuelekea mwezi wa 10 Mtandao huo ulibadilisha jina lakini hawakubadilisha homepage yaani muonekano wa ukurasa wa mwanzo.

Mwanzoni waliita OnlineTaskPay, hapo chini walibadilisha wakiita Money4Task.

Baada ya kufikia mwezi wa 9 mwishoni sasa wamebadilisha jina na kuuita mtandao huu Youthnize ambapo muonekano wa mtandao huu ni wa aina ile ile.

Ukurasa wa Youthnize Sasa mwanzoni mwa mwaka 2017 mtandao huu umebadilishwa na kuitwa Revenue Brust ukiwa na muonekano tofauti wa kuvutia kuliko ule wa mwanzo.

Ukurasa mpya wa Revenue Brust.
Kumbuka unapojisajili unatakiwa kuweka Email yako na hiyo ndiyo inyotumika kudukua taarifa zako ambapo ni rahisi hata kukuibia endapo baadae utaambiwa utoe namba yako ya bank ili wakutumie hela kitu ambacho wakati wa uchunguzi watu tumekishuhudia.

Nini malengo hasa ya mitandao hii?
Ni kweli kabisa kwamba malengo ya mitandao hii haina tija kwa mtumiaji. Lakini napenda kukiri kuwa huenda kuna ambao wamelipwa hayo mamilioni ya bure kila mwezi. Hata hivyo tungependa kutoa fursa kwa ambao tayari wamelipwa watoe ushahidi. Hakuna asiye penda hela tena ya kupata ukiwa umelala.

Malengo makubwa ya mitadao hii ni kuwanufaisha wanaomiliki mtandao na kuiba taarifa za mtumiaji.

Wanafaidika vipi?
Kwa kuwa watu wengi hutembelea mitandao hiyo, huwa inapata traffic kubwa ambayo baadae traffic hiyo huamishwa kwenye site ambayo hutengenezwa hivyo kufanyia biashara ya Online Advertisements ambapo huingiza kipato kikubwa kwa njia ya pay per impression/view yaani kitaalmu PPV.

Mfano mzuri ni mtandao wa Youthnize ambao umekuwa Website ya Entertainment iitwayo Youth Nize na kupata traffic kubwa kwa muda mfupi kwa kutumia traffic ya Youthnize ambayo watu wengi waliitembela kipindi hicho ukiwa ni mtandao wa mihela.

Wanaibaje?
Kupitia taarifa wanazokuomba ili wakulipe fedha kama umeshafikisha fedha tajwa kitaalamu inajulikana kama Threshold huwa wanakuomba uwape namba za akaunti ya benki ili wakuingizie hela. Kadi lazima iwe ya kimataifa mfano Visa, MsterCard au American Express n.k. Hapo watakwambia uwape namba za kadi pia na namba 3 za mwisho za activation. Hapo ndio mwanzo wa kuliwa unapoanza.

Uongo kwa watumiaji.

Watu wengi wanaotumia mitandao hii huwa ni waongo kwamba wamelipwa. Ukweli ni kwamba sisi hatuna ushahidi wa aliyelipwa. Isipokuwa watu wengi wanaowashawishi watu wabonyeze link zao huwa wanawaambia kuwa wamelipwa kama njia ya kuwashawishi. Katika hali ya kawaida siyo rahisi fedha ya miaka hii ikapatikana kirahisi kiasi cha namna hii. Tufanye kazi Watanzania tusilimbuke na mitandao ya kijamii.
 
Back
Top Bottom