Salamu yangu kwenu siku ya leo inatoka
2 Wafalme 4:26
[26]Tafadhali piga mbio sasa kwenda kumlaki, ukamwambie, Hujambo? Mume/mke wako hajambo? Mtoto/watoto wako hawajambo? Akajibu, Hawajambo.
Kama jibu lako nawe ni hawajambo, Mungu wa mbinguni aendelee kukupa uheri wa afya wewe na wote niliotaka hali zao hapo juu.
Kama jambo haipo, naachilia kwako amani ya Mungu wangu ipitayo amani zote ndani yako, na Mungu afanye uharaka katika kuponya kwa yote yanayoku/wasibu.
Moja kwa moja kwenye somo.
Aya kuu
2 Samweli 15:11
[11]Na watu mia mbili walioalikwa wakatoka Yerusalemu pamoja na Absalomu, wakaenda katika ujinga wao wasijue neno lo lote.
Utangulizi
Kutakuwa na mafunzo yasiyopungua matano katika somo hili, mafunzo hayo yote hayatakuja kwa siku moja, bali kila funzo litatoka kwa siku yake. Mafunzo yote hayo yatajengwa kupitia 2 Samweli 11 - 2 Samweli 18.
Kumbuka: Ili twende sambamba katika somo hili, unatakiwa kufanya moja kati ya mambo mawili.
Jambo la kwanza: Soma mwenyewe (2 Samweli 11 - 2 Samweli 18).
Jambo la pili: Fuatana nami katika muhtasari wa (2 Samweli 11 - 2 Samweli 18)
Kushindwa kufanya mojawapo kati ya mambo mawili hapo juu, ni ishara ya kufuatana nami kiupofu pofu (kuambulia sifuri katika mafunzo yote nitakayoleta katika uzi huu)
Funzo namba moja litakujia kesho saa 2:00 usiku.
Muhtasari
Tunaanza hivi
Absalomu alikuwa mtoto wa kwanza kwa mama yake japo si wa kwanza kwa baba yake mfalme Daudi. Wakati mfalme Daudi alipotenda kosa la kumchukua kinguvu mke wa Uria mhiti aliyeitwa Bath-sheba (soma 2 Samweli 11), Mungu alimwahidi jambo lifuatalo: -
2 Samweli 12:10-12
[10]Basi, sasa upanga hautaondoka nyumbani mwako, kwa sababu umenidharau, ukamtwaa mkewe Uria, Mhiti, kuwa mke wako.
[11]BWANA asema hivi, Angalia, nitakuondokeshea uovu katika nyumba yako, nami nitawatwaa wake zako mbele ya macho yako, na kumpa jirani yako, naye atalala na wake zako mbele ya jua hili.
[12]Maana wewe ulifanya jambo lile kwa siri; bali mimi nitalifanya jambo hili mbele ya Israeli wote na mbele ya jua.
Namna upanga ulivyoinuka
Amnoni, mtoto wa kiume wa kwanza wa mfalme Daudi, alimbaka na kumbikiri umbu (dada) wa Absalomu aliyeitwa Tamari (soma 2 Samweli 13 : 1 - 22).
Absalomu akimbilia Geshuri
Baada ya kubakwa kwa umbu lake, aliaanda mkakati wa kumwangamiza kaka yake Amnoni, mpango aliofanikiwa kuukamilisha baada ya miaka miwili (soma 2 Samweli 13 : 23 - 39). Baada ya kumuua Amnoni, alikimbilia huko Geshuri kwa mfalme Talmai mwana wa Amihuri, alifanikiwa kukaa huko kwa miaka mitatu. Yoabu aliyekuwa kamanda wa majeshi ya Israeli kwa wakati huo, alitambua namna mfalme alivyokuwa anampenda Absalomu lakini akiwa amekosa namna ya kumrudisha, ndipo alisuka mkakati wa kumrudisha ndani ya Israeli (soma 2 Samweli 14). Lakini baada ya kurudi kwa Absalomu, mfalme Daudi hakutaka kuzungumza naye mpaka tu pale Absalomu alipolazimika kuchoma shamba la Yoabu ndipo akafanikiwa kuongea na mfalme (soma 2 Samweli 14 : 28 - 33).
Absalomu aandaa mpango wa kumpindua mfalme
Baada ya kufanikiwa kuonana na mfalme Daudi, Absalomu aliandaa uasi wa waisraeli kwa mfalme Daudi, na biblia inatujulisha yafuatayo.
2 Samweli 15:1-12
[1]Ikawa baada ya hayo, Absalomu akajiwekea tayari gari na farasi, na watu hamsini wa kupiga mbio mbele yake.
[2]Tena Absalomu huondoka asubuhi na mapema, na kusimama kando ya njia ya lango; kisha ikawa, mtu ye yote aliyekuwa na neno, lililokuwa halina budi kufika kwa mfalme ili kuhukumiwa, Absalomu humwita mtu huyo kwake, na kumwuliza, Wewe u mtu wa mji gani? Naye akasema, Mtumwa wako ni mtu wa kabila fulani ya Israeli.
[3]Naye Absalomu humwambia, Tazama, maneno yako ni mema yenye haki; lakini hapana mtu aliyeagizwa na mfalme kukusikiliza.
[4]Tena Absalomu husema, Laiti mimi ningewekwa kuwa mwamuzi katika nchi hii, ili kila mtu mwenye neno au daawa aje kwangu, nimpatie haki yake!
[5]Tena ikawa hapo alipokaribia mtu ye yote kumsujudia, hunyosha mkono wake, na kumshika, na kumbusu.
[6]Hivyo ndivyo Absalomu alivyowatendea Israeli wote, waliomwendea mfalme ili wapate hukumu; na hivyo Absalomu akawadanganya watu wa Israeli.
[7]Hata ikawa mwisho wa miaka minne, Absalomu akamwambia mfalme Tafadhali uniache niende nikaondoe nadhiri yangu, niliyomwekea BWANA huko Hebroni.
[8]Maana mimi mtumishi wako naliweka nadhiri hapo nilipokuwa nikikaa Geshuri katika Shamu, nikasema, Kama BWANA akinirudisha Yerusalemu kweli, ndipo nitamtumikia BWANA.
[9]Naye mfalme akamwambia, Enenda na amani. Basi akaondoka, akaenda Hebroni.
[10]Lakini Absalomu akapeleka wapelelezi katika kabila zote za Israeli kusema, Mara mtakaposikia sauti ya tarumbeta, ndipo mtakaposema Absalomu anamilikl huko Hebroni.

[12]Absalomu naye akatuma kumwita Ahithofeli Mgiloni, mshauri wake Daudi, kutoka katika mji wake, yaani, Gilo, alipokuwa akitoa dhabihu. Fitina yao ikawa na nguvu; maana watu waliokuwa pamoja na Absalomu wakazidi kuwa wengi.
Daudi akimbia Yerusalemu
Soma 2 Samweli 14 : 13 - 31
Daudi aomba Mungu kuvuruga ushauri wa Ahithofeli kwa Absalomu
2 Samweli 15:31
[31]Mtu mmoja akamwambia Daudi ya kwamba, Ahithofeli yu katika hao waliopatana na Absalomu; Daudi akasema, Ee BWANA, nakusihi, uligeuze shauri la Ahithofeli liwe ubatili.
Daudi atuma mpelelezi kwa lengo la kuvuruga ushauri wa Ahithofeli kwa Absalomu
2 Samweli 15:32-37
[32]Ikawa, Daudi alipofika juu, hapo Mungu alipoabudiwa, tazama, Hushai, Mwarki, akaja kumlaki na joho lake limeraruliwa, tena ana udongo kichwani mwake.
[33]Daudi akamwambia, Ukienda mbele pamoja nami, utakuwa mzigo kwangu;
[34]lakini ukirudi mjini, na kumwambia Absalomu, Nitakuwa mtumishi wako, Ee mfalme; kama vile nilivyokuwa mtumishi wa baba yako tokea zamani, ndivyo nitakavyokuwa mtumishi wako sasa; ndipo utayavunja mashauri ya Ahithofeli kwa ajili yangu.
[35]Je! Hawako Sadoki na Abiathari, makuhani, pamoja nawe huko? Basi itakuwa, kila neno utakalolisikia katika jumba la mfalme, utawaambia Sadoki na Abiathari, makuhani.
[36]Angalia, wanao huko pamoja nao wana wao wawili, Ahimaasi, mwana wa Sadoki, na Yonathani, mwana wa Abiathari; nanyi kwa mikono yao mtanipelekea habari ya kila neno mtakalolisikia.
[37]Basi Hushai, rafiki wa Daudi, akaingia ndani ya mji; naye Absalomu akafika akaingia Yerusalemu.
Ushauri wa Ahithofeli kwa Absalomu
2 Samweli 17:1-4
[1]Zaidi ya hayo Ahithofeli akamwambia Absalomu, Niache nichague watu kumi na mbili elfu, nami nitaondoka na kumfuatia Daudi usiku huu;
[2]nami nitamshambulia wakati atakaokuwa amechoka, na mikono yake imekuwa dhaifu, nami nitamtia hofu; na watu wote walio pamoja naye watakimbia; nami nitampiga mfalme peke yake;
[3]na hao watu wote nitawarejeza kwako; mtu yule umtafutaye ni kana kwamba wamerudi wote; na hivyo watu wote watakuwa katika amani.
[4]Shauri hili likawa jema machoni pa Absalomu, na machoni pa wazee wote wa Israeli.
Ushauri wa mvuruga ushauri (Hushai Mwarki)
2 Samweli 17:5-14
[5]Ndipo Absalomu akasema, Basi, mwiteni Hushai, Mwarki, naye, tukasikie atakayosema yeye pia.
[6]Basi Hushai alipofika kwa Absalomu, Absalomu akamwambia, akasema, Ahithofeli amesema hivi; je! Tufanye kama alivyosema? Kama sivyo, sema maneno yako.
[7]Hushai akamwambia Absalomu, Shauri hili alilolitoa Ahithofeli si jema wakati huu.
[8]Hushai akafuliza kusema, Wamjua baba yako na watu wake, ya kuwa ni watu mashujaa hawa, nao wana uchungu katika mioyo yao, kama dubu aliyenyang’anywa watoto wake nyikani; tena baba yako ni mtu wa vita, hatalala pamoja na watu wake.
[9]Angalia, amefichwa sasa katika shimo, au penginepo; kisha itakuwa, watakapoanguka baadhi yao mwanzo, kila mtu atakayesikia, atasema, Kuna machinjo katika watu wanaofuatana na Absalomu.
[10]Basi hata yeye aliye shujaa, mwenye moyo kama moyo wa simba, atayeyuka kabisa; maana Israeli wote wanajua ya kuwa baba yako ni shujaa, na ya kuwa watu wale walio pamoja naye ni mashujaa.
[11]Kwa hiyo shauri langu ni hili, Waisraeli wote toka Dani mpaka Beer-sheba wakusanyike kwako, kama mchanga wa bahari kwa wingi; na wewe uende vitani mwenyewe.
[12]Hivyo tutamfikia mahali po pote atakapoonekana, na kumwangukia kama vile umande uangukavyo juu ya nchi; wala hatutaacha hata mmoja wao, yeye na watu wote walio pamoja naye.
[13]Tena, ikiwa amejitia katika mji uwao wote, basi Israeli wote wataleta kamba, na kuuendea mji ule, nasi tutaukokota mpaka mtoni, wala halitaonekana huko hata jiwe dogo moja la mawe yake.
[14]Naye Absalomu na watu wote wa Israeli wakasema, Shauri la Hushai, Mwarki, ni jema kuliko shauri la Ahithofeli. Kwa maana BWANA alikuwa amekusudia kulivunja shauri jema la Ahithofeli, ili BWANA alete mabaya juu ya Absalomu.
Hushai Mwarki amtahadharisha Daudi
2 Samweli 17:15-16
[15]Ndipo Hushai akawaambia Sadoki na Abiathari, makuhani, Ahithofeli amempa Absalomu na wazee wa Israeli mashauri kadha wa kadha; na mimi nimetoa mashauri kadha wa kadha.
[16]Basi sasa pelekeni habari upesi kamwambieni Daudi ya kwamba, Usilale usiku huu karibu na vivuko vya jangwani; bali usikose kuvuka; asije akamezwa mfalme, na watu wote walio pamoja naye.
Kufariki kwa Ahithofeli
2 Samweli 17:23
[23]Naye Ahithofeli alipoona ya kuwa shauri lake halikufuatwa, akatandika punda wake, akaondoka, akaenda nyumbani kwake, mjini mwake, akaitengeneza nyumba yake, akajisonga; akafa, akazikwa kaburini mwa babaye.
Absalomu na baadi ya watu waliomfuata wauawa
2 Samweli 18:6-8
[6]Hivyo watu wakatoka waende nyikani ili kupigana na Israeli; na vita vikatokea ndani ya msitu wa Efraimu.
[7]Watu wa Israeli wakapigwa huko mbele ya watumishi wa Daudi, kukawa na maangamizo makuu huko siku ile, ya watu ishirini elfu.
[8]Kwa maana vita vilienea huko juu ya uso wote wa nchi; na siku ile huo msitu ukala watu wengi kuliko wale walioliwa na upanga.
2 Samweli 18:9-17
[9]Na kwa bahati Absalomu akakutana na watumishi wa Daudi. Naye Absalomu alikuwa amepanda nyumbu wake, na yule nyumbu akapita chini ya matawi manene ya mwaloni mkubwa, hata kichwa chake kikakwama katika mwaloni huo, akanyakuliwa juu kati ya mbingu na nchi; na yule nyumbu aliyekuwa chini yake akaenda mbele.
[10]Basi mtu mmoja akaona hayo, akaenda akamwambia Yoabu, akasema, Tazama, mimi nalimwona Absalomu ametundikwa katika mwaloni.
[11]Naye Yoabu akamwambia mtu yule aliyempasha habari, Je! Wewe umeona haya; Mbona, basi, hukumpiga hata nchi papo hapo? Nami ningalikupa fedha kumi na mshipi.
[12]Yule mtu akamwambia Yoabu, Kama ningalipata fedha elfu mkononi mwangu, hata hivyo singalinyosha mkono wangu juu ya mwana wa mfalme; kwa maana mfalme masikioni mwetu alikuagiza wewe, na Abishai na Itai, akisema, Angalieni sana mtu awaye yote asimguse yule kijana, Absalomu.
[13]Na tena, kama ningaliitendea roho yake kwa hila; (wala hapana neno lo lote liwezalo kufichwa mbele ya mfalme); ndipo wewe mwenyewe ungalijitenga.
[14]Ndipo Yoabu akasema, Siwezi kungoja na kusema nawe hivi. Akachukua vyemba vitatu mkononi mwake, akamchoma Absalomu moyoni, alipokuwa akali hai katikati ya ule mwaloni.
[15]Kisha vijana kumi, waliomchukulia Yoabu silaha zake wakamzunguka, wakampiga Absalomu, na kumwua.
[16]Kisha Yoabu akapiga tarumbeta, wakarudi watu toka kuwafuatia Israeli; kwani Yoabu akawazuia watu.
[17]Nao wakamtwaa Absalomu wakamtupa katika shimo kubwa mle msituni, wakaweka juu yake chungu kubwa sana la mawe; kisha Israeli wote wakakimbia kila mtu hemani mwake.
Asante kwa kuwa nami siku hii ya kwanza katika kuangazia kwa muhtasari yale ambayo kutoka kwayo tutakuwa na mafunzo kadha wa kadha.
Tukutane kesho saa 2:00 usiku kwa funzo namba moja.