Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,997
- 20,329
Binadamu ana sehemu kuu tatu tu za maisha yake, maisha ya kuzaliwa, maisha ya ndoa, na mwisho kifo!
Kamanda Malisa GJ ameingia leo katika maisha ya ndoa, ni ulimwengu wa pekee wenye kukusanya tamaduni, tabia na mila za aina mbili na kuzifanya ziunde tamaduni moja yenye nguvu. Wizara hii ni Ngumu inahitaji hekima, maarifa na akili ya kuzaliwa. Wapo maprofesa wamefeli, wapo madaktari wamefeli, wapo wajinga na maamuma wamefaulu.
Ndoa haina darasa, ndoa haina mwalimu, Wengi wajiitao walimu wa ndoa, wao ndoa zao hulala na mapanga mkononi...
Malisa ndugu yangu, ndoa ni wewe na mkeo kipenzi Doreen, kamwe hatatokea muongozaji au mwelekezaji au muamuzi wa ndoa yenu, isipkuwa ni wewe na mkeo ndio wenye kura ya veto. Utamu na uchungu wa ndoa yenu utaanza kuuona leo, wote waliojaa na kuserebuka leo ndio watakaoibomoa ndoa yenu ikiwa mtaruhusu waendelee kuserebuka katika ndoa yenu.
Zingatia baada ya ndoa usiku huu makutano wote watarudi kwao, na kwaushahidi mdogo, fikiria kwenye shamrashamra zote usiku huu, kuna mtu alitaka kujua kesho yenu kiroba cha unga mtakipataje?
Amini wewe sasa ni mwanamume sio mwanaume tena, wewe ndio baba wa mkeo na yeye ndio mama wa wewe, huna pakushitakia machungu au furaha zako zaidi ya kwa mkeo kipenzi Doreen, nae hana pakushitakia machungu yake au furaha yake zaidi ya kwako.
Umebeba agano la mkeo Doreen, naye kabeba agano lako, Usituruhusu marafiki tuijue ndoa yako, na mkeo asiruhusu marafiki waijue ndoa yake!
Lakini nikung'ate sikio rafiki yangu, mwanamke siku zote sauti yake huelekea juu mawinguni na hasa awapo na mashoga zake vicheko vyake huwa na sauti nyembamba kali iendayo juu... Ulishawahi kujiuliza? Naam, basi na sharti mwanamume sauti yake iende chini, tena chini ardhini kifuani... Ndio thamani ya kifua cha mwanamume!
Silaha yako katika ndoa ipo katika zipu, magoti na neno samahani!
Nikutakie kilala kheri katika ndoa yenu, utaendelea kujifunza kwa wenye ndoa wema tu na sio kila ndoa ni kioo kwako, zingine ni laana!
Na Yericko Nyerere