Ushindi wetu mkubwa kupita zote ni Katiba Mpya

Sep 16, 2017
22
87
Habari za asubuhi ndugu wapenda haki.

Nimekuwa nikifuatilia taarifa na matukio mbali mbali yanayoendelea hapa nchini kwa muda mrefu sana, ni dhahiri shahiri kuwa tuna kila sababu ya kuungana na kuongea lugha moja kama taifa, matatizo yote yanayoendelea ukiyaangalia kwa jicho la karibu kiini chake ni mzizi uliojikita chini zaidi wala sio matawi kama watu wengi wanavyodhania.

Tumekuwa na vyama vya upinzani vingi sana zaidi ya 22 na mchango wake tumeuona kwa kipindi cha nyuma kwa kiasi Fulani lakini tunashuhudia anguko kubwa sana ambalo sio la kiutashi bali la lazima, hapa kuna jambo la kujifunza tena kubwa kwani tuna kila sababu ya kufanya tafakuri ya kina ili kuona namna ilyo salama na yenye tija kwa ustawi wa jamii yetu.

nimeenda mbali na kuwaza utashi wa kweli wa vyama vya upinzani ni upi, ni maendeleo ya nchi na wananchi kupitia demokrasia iliyo ya kweli au ni sehemu yao ya kupata mkate wa kila siku? majibu yanayokuja kichwani yananichanganya sana tena sana. najiuliza swali dogo sana kwamba, unawezaje kupata haki ndani ya sanduku la kura hali ukijua kwamba wanaosimamia uchaguzi ni wateule wa mkuu, wanaolinda usalama ni vyombo vinavyowajibika kwa mkuu wa kaya? uanwezaje kupata ushindi katika mazingira kama haya? kama kweli tumedhamiria demikrasi ni kwanini nguvu zetu tusiziwekeze kwenye kushinikiza tume huru ya uchaguzi? ni kwanini tusitengeneze awareness ya wananchi wetu na kuratibu mipango yenye kufuta haki na sharia za nchi ili kudai katiba mpya ya wananchi kuliko hii inayompa madaraka makubwa mkuu wa nchi?

Nadhani wakati sahihi ni huu wa kuamka na kuidai katiba, yanayotokea sasa ni mambo ambayo impact zake zitaonekana in a long run na waanga wakubwa ni sisi.

KATIBA MPYA NDO UTAKUWA MSINGI WA HAKI KWA WANANCHI WOTE, KATIBA MPYA NDO ITALETA MGAWANYO SAWA WA MALIASILI ZA NCHI. NGUVU NA AKILI ZETU NAPESA TUZIWEKEZE HAPA NA SIO KUTAFUTA MADARAKA KWA SASA. MSINGI KWANZA.

Imeandikwa na
James Rutasitara
 
umenena vyema mkuu.... bila kushinikiza katiba mpya tutaendelea kuitwa wapiga madili.
 
Kabisa mkuu,katiba bora italeta mifumo na taasisi imara,checks&balance. Sasa inabidi tumuombee sana JPM kwa kuwa tamko lake laweza leta athari kubwa
 
Ila me binafsi napata kigugumizi kuamini kwamba katiba mpya ndyo muarobaini wa matatzo yetu kama taifa, coz vingoz wetu tulionao hawana hulka ya kuheshimu katiba za nchi zao wala sheria walizo jiwekea, kwa mfano awamu hii katiba ipo lakini haifuatwi, hivyo nadhani kikukubwa na cha msingi ni kujenga utamaduni wa kuwawajibisha viongozi wetu tuliowachagua wakikosea tuwa kemee bila uwoga.
 
Back
Top Bottom