Mimi ni kijana mtanzania mwenye umri wa miaka 24, mzaliwa wa kijiji cha Butiama, mkoani Mara. Nina shahada ya kwanza ya sayansi ya mazingira na usimamizi (BSc.Environmental science and Mangement) ya chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine (SUA). Kwa sasa ninafanya kazi katika kampuni binafsi (environmental laboratory) kama mkemia wa wazingira (Environmental chemist).
Ingawa sina jina kubwa kisiasa na wala sitoki katika familia inayofahamika (mtoto wa mkulima), lakini najitambua kama mtanzania kijana mwenye uzalendo na utaifa wa kweli pia nayatambua matatizo ya watanzania wa jimbo la Musoma(v).
Nina ndoto kubwa ya kutaka kuwatumikia watanzania wenzangu ambao walichangia kwa namna moja au nyingine mpaka nimefikia hapa. Sasa naona ni wakati muafaka wa mie kuwatumikia na kuwaletea tumaini jipya, so nina ndoto za kuomba ridhaa ya kupeperusha bendara ya chama changu (CHADEMA)- 2015, ili kupata ridhaa ya wananchi wa jimbo la Musoma Vijijini (Butiama) kuwa muwakilishi wao mjengoni
Nina uwezo wa kujenga hoja na kuzisimamia, nina uwezo wa kuyatambua, kuyatafsiri na kutoa mbinu za kuyatatua matatizo ya wananchi wangu bila kukinzana na sera ya chama na kwa manufaa ya chama na umma kwa ujumla.
Pia nina karama ya uongozi kwan katika makundi yote ambayo nshawahi kupitia, kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu nimekuwa kiongoz wa wenzangu kwa nyanja mbalimbali, na kwa neema ya Mungu nilifanya vizur katika kila jukumu nililopewa na wenzangu kuwatumikia.
Wadau naombeni ushauri wenu wa dhati kuhusu uamuzi wangu lakin pia ni nn kifanyike ili kwa pamoja 2weze kulikomboa jimbo la Musoma vijijini, ambalo kwa sasa lipo chini ya Mh. Mkono (CCM)
Nawaclisha