Superb2014
JF-Expert Member
- Jul 29, 2017
- 10,404
- 8,698
Dada na mdogo wangu, pole kwa yote. Nianze kukushauri kwamba huna haja ya kuamini maneno ya wifi yako kwani yeye sio Mzazi wala Mungu. Ila kuhusu maisha magumu wengi wanapitia na hasa kipind hiki kila mtu analalamika kivyake. Kama unajua wifi yako hawataki mwacheni fanyenyeni kazi mfanye maisha yenu kwani nyie hamna pa kuishi? Waachacheni na ndoa yao.Salamu kwenu wana JF wote.
Katika maisha ya kila siku tukiwa kama Binadamu tunakutana na changamoto nyingi. Miaka kama 8 iliyopita kuna ugomvi ulitokea kati yangu na Wifi yangu yaani Mke wa Kaka yangu, huyu Wifi yangu ni mtu mwenye hasira sana, kinyongo na anapenda kuzusha maneno ya uongo na anapenda sana ugomvi kwa kifupi hapendi Ndugu wa Mume na Mume wake analitambua hilo.
Katika ugomvi huo aliniambia kuwa nitaishi maisha ya shida, ukweli ni kwamba maisha yangu yamekuwa ya shida kama alivyotamka.
Naomba ushauri je huyu Wifi yangu atakuwa ni mtu wa aina gani? Je nifanye nini ili niweze kutatua hii changamoto? Maana kama ni maombi nimefanya sana maombi.
Kwa niaba ya Rafiki yangu naomba kuwakilisha.
Dada na mdogo wangu, pole kwa yote. Nianze kukushauri kwamba huna haja ya kuamini maneno ya wifi yako kwani yeye sio Mzazi wala Mungu. Ila kuhusu maisha magumu wengi wanapitia na hasa kipind hiki kila mtu analalamika kivyake. Kama unajua wifi yako hawataki mwacheni fanyenyeni kazi mfanye maisha yenu kwani nyie hamna pa kuishi? Waachacheni na ndoa yao.
Tafuta shughuli ya kukuingizia kipato kama huna ili muondoe utegemezi kwa kaka yenu.
Achana na ugomvi sio kitu kizuri hakimpendezi Mungu, kuomba kwako na hata ukifunga itakuwa ni kazi bure kama huwezi achilia moyoni ugomvi na chuki.
Wapendeni maadui zenu waombeeni wanaowatesa. Ni kauli yake Yesu kwetu wanadamu.
Fanya maombi bila kuchoka eti miaka nane unasema umeomba hadi umechoka? Mbona hasira juu ya wifi yako miaka 8 hauchoki kizitunza kifuani mwako.?
Nikusihi tu maisha mazuri hayaji kwa maombi tu pia ufanye kazi, usione aibu kupitia kazi ndogo na za aibu utainuliwa sana. Ipo siku utatabasamu. Mungu akutie nguvu ya roho na mwili.
Ugumu wa maisha upo kwa wote jamani hasa hii awamu ya5. Kwa hiyo tuvumilie tu na kutafufa namna mbadala ya kulainisha vyuma kama grisi imeshindwa. Tusitafute sababu
Shida unayo wewe mkuu kwakutokuachilia hasira uliyonayo juu yake kiasi chakuona kila jambo lako limefungwa kwenye kinywa cha wifi yako,samehe utakua huru
Asante kwa ushauri.Uamuzi wa kuishi maisha ya shida au raha yako mikononi mwako. Unapoishi kwa kufikiria eti wifi alisema nitakua na maisha ya shida happy ndipo unapojichulia bila kujua. Chakufanya weww mpuuze Kama like Kama umekutana na kichaa balabalani akakwambia utaishi kwa shida . Huyo ni kichaa tu . Wewe tazama maisha yako Kisha jipangie mipango yako vizuri Kisha songa mbele
Ni wewe umeamua yawe ya shida
Kimsingi hayo maneno ya wifi yako hayana effect yoyote katika maisha yako
Kwani maisha yako yamekuwa ya shida katika jambo gani?
Pambana ndugu,riziki ya mja haizibwi na mtu yeyote.funga na kusali uku ukipambana........Mungu atafungua njia
fanya kazi, acha kutafuta mchawi ni nani.
tafuta kazi ufanye wewe.....shida hazitatuliwi na umbeya......