kijana mkimya
JF-Expert Member
- Sep 10, 2015
- 277
- 121
Huyu dada ameolewa huko nchi za watu, miaka 7 ndoani ana watoto wawili. tatizo alilokuwa nalo dada anataka kurudisha makazi Tanzania mume wake hataki (jamaa ni raia wa hiyo nchi).
Ugumu unakuja huyu dada anataka kurudi Tanzania na watoto wake jamaa hataki, anamwambia kama unataka kurudi arudi aache watoto, hawezi kuwaruhusu watoto wake waje kuishi Africa.
Watoto wana uraia wa hiyo nchi, ameenda kwenye vyombo vya sheria vya huko, dizaini kama wanamletea ukauzu fulani, wanamwambia ili apate ruhusa ya kuchukua watoto inabidi akubaliane na jamaa, ukiangalia jamaa hataki kabisa kusikia habari za kuishi Africa.
Huyu dada ni Engineer, anafanya kazi huko, anasema wanalipa vizuri tu. Nimejaribu kumpeleleza sababu za yeye kutaka kurudi Tanzania anasema amechoka kuishi huko, anataka kuja karibu na ndugu zake (kutokana na maongezi yake naona hii sababu si ya kweli kuna sababu nyingine hataki kusema) anasema anataka kurudi Tanzania lakini hataki kuwaacha watoto huko.
Hebu msaidieni huyu dada, mi nimeshindwa kumpa ushauri, kwanza sababu anayotoa siamini kama ina ukweli. Watu wa sheria mnamshauri vipi huyu dada yetu, hataki kabisa kuendelea kuishi huko na hataki kuacha watoto huko ndoa ilifanyika huko huko.