Wazima humu??
Ni hivi nina, rafiki yangu amepatwa na janga, nimeona nililete huku kwa wazee wa busara maana ni kama nimeshindwa hivi kumpa ushauri sahihi...
Jamaa baada ya kumaliza form 6 akaenda kupiga tempo shule fulan hv mkoani huko, akiwa kule alikutana na dada mmoja hivi wakaanzisha mahusiano, yule dada alikuwa mdogo mdogo km miaka 16 hivi, na pale alikuwa anaishi kwa mama yake,. And kwa kipindi kile alikuwa hasomi, lakin kumbe alikimbia kwa dada yake ili aishi na mama yake, na kipindi yupo kwa dada yake alikuwa anasoma ila baada ya kutorokea kwa mama yake akaacha shule, so jamaa alikutana naye miezi 3 tangu aache shule kwa dada na kuja kwa mama.
Jamaa akawa anatafuna tunda huku anapiga tempo kusubiri tokeo la kidato cha 6, mchezo ukanoga jamaa akamtwisha mimba yule dada, mama yake hakuwa na neno akaomba tu ahudumie mimba, Mara paap matokeo yakatoka na akawa amesimamisha kijiti cha 8 PCB, muda wa chuo ulipofika akaaga vizuri tu akaenda zake kupiga pharmacy chuo fulan hapa nchini, mama mjamzito akabaki kwa mama yake mzazi wakaagana kwa baraka zote akasisitizwa asisahau kama ameacha mjamzito mwenye mtoto wake tumboni.
Jamaa akiwa chuo alijitahid kutuma kidogo akipatacho, sasa baada ya miezi 3 hivi habari za ujauzito zikamfikia yule dada wa binti, hapo ndo mambo yakawa mengi, dada akampigia simu mshikaji na kuanza kumpiga mikwara ya hatari sana na kwamba anafungua kesi polisi kumshitaki jamaa amempa mimba mdogo wake akiwa mwanafunzi, jamaa akajaribu kujieleza na kuahidi kwamba atamuoa yule binti dada mtu akakaza hasa , mshikaji akaamua kukata mawasiliano, akabadili namba ya simu, wakapotezana kabisa na mwanamke wake.
Miaka ya chuo ikaisha akarudi mtaani akapata kazi, akaamua kufuatilia mtoto wake, anakuja kuambiwa kuwa yule dada baada ya kuona jamaa hapatikani na dada ni mkali Kama mbogo, masimango hayaishi kila kukicha akaamua kutoroka na mtoto wake, walipofuatilia ikaja kubainika alitoroka na mwanaume mmoja hivi mzee na wameelekea Msumbiji, simu yake haipatikani kabisa, jamaa yupo hoi kbs, anampenda Yule mwanamke na anampenda mtoto wake.
Ushauri achukue hatua gani kuipata familia yake??
Pia, amenambia amesikia kwa watu kuwa dada bado ana nia ya kumshtaki jamaa siku yoyote atakayoonana naye, yupo njia panda sana,. Je bado anashitakika??
Na Kama anashitakika, afanyeje Sasa??
Msaada waheshimiwa....