Ushauri wa kisaikolojia kuhusu COVID-19

Ushauri wa kisaikolojia kuhusu COVID-19

CalvinKimaro

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2017
Posts
245
Reaction score
314
Mshauri mmoja wa mambo ya saikolokjia na jamii aliyefuatilia mlipuko wa Corona unaosababishwa na Virusi vya Covid-19 ameshauri ifuatavyo:

1. Jitenge mwenyewe usipate taarifa mbaya za ugonjwa huu kila mara (kwa kuwa mambo mengi unayohitaji kujua juu ya Corona umeshayajua, yaliyobaki ni marudio tu)

2. Usitafute habari za vifo. Huu sio mchezo wa mpira kwamba unataka kujua matokeo: mumeshinda ngapi au mmefungwa.

3. Usitafute habari za nyongeza kwenye mitandao. Zitanyong’onyeza hali yako ya afya ya akili. Kujua namna ugonjwa unavyoathiri kunakuongezea Msongo wa mawazo na woga.

4. Epuka kutuma ujumbe wenye taarifa mbaya ya corona. Wengine wana udhaifu mkubwa kwenye uwezo wao kuhimili habari mbaya (badala ya kuwasaidia unaweza kuwasababishia madhara ikiwemo msongo wa mawazo).

5. Ikiwezekana kaa nyumbani na usikilize muziki kwa sauti laini katika hali tulivu. Tafuta michezo ya kuburidisha watoto na familia. Simulia hadithi, angalia sinema au hata vipindi vya ucheshi. Usiache kuzungumzia mipango yako ya baadae na ya kifamilia.

6. Tunza nidhamu nyumbani kwako haswa ya utaratibu wa usafi kuepuka maambukizi. Nawa mikono kwa sabuni mara kwa mara na uwafuatilie wote nyumbani wafanye hivyo.

7. Kuwa na mtazamo chanya kunaimarisha hali ya kinga ya mwili huku mtazamo hasi unaweza kuchangia msongo wa mawazo na kuharibu kinga ya mwili wako. Pia mtazamo wako chanya utawajengea matumaini unaoishi nao nyumbani kwako.

La muhimu zaidi ni kuamini kuwa hata hili litapita! Na kwamba wewe na jamii yako mtakuwa salama

IBADA : SALA NA KUSOMA MAANDIKO MATAKATIFU PIA NYUMBANI KWAKO NI MUHIMU KUONDOA STRESS. KUMBUKA HUJAWAHI KUJILETA WEWE DUNIANI, NI KUDRA TU ZA MWENYEZI. JIKABIDHI KWAKE, NA MWOMBE ULINZI, MWAMBIE YEYE AJUAYE MWANZO WAKO, NDIYE PEKEE AKAHUSIKE NA HATMA YAKO HAPA DUNIANI.

# Stop panic, StayPositive
#StaySafe, protect your family and others!!
 
Covid ipo na inauuwa na tunaambiwa ni pneumonia🤣🤣🤣🤣
 
Afya ya kisaikolojia ni muhimu sana kipindi hiki, kuna kitu kinaitwa panic disorder, kuna jamaa alipata hilo shambulio alitupigia simu kuaga anasema COVID-19 ndio imemuanza, anakata moto, tulihangaika sana mpaka kumtuliza.
top-symptoms-of-panic-attacks-2584270_FINAL-5bcdfd4d46e0fb0051228ee5.png
 
Uoga unaua, mi niliambiwa hosp. yetu hapa kuna korona majuzi kati nikaenda muona mgojwa tangu nimetoka nikawa nahisi eti naumwa hadi mawazo yalipo isha ndo najiona sawa
 
Hii kitu ni muhimu sana nilifanya hivyo toka last year, taarifa nyingi zinaongeza hofu.
 
Mshauri mmoja wa mambo ya saikolokjia na jamii aliyefuatilia mlipuko wa Corona unaosababishwa na Virusi vya Covid-19 ameshauri ifuatavyo:

1. Jitenge mwenyewe usipate taarifa mbaya za ugonjwa huu kila mara (kwa kuwa mambo mengi unayohitaji kujua juu ya Corona umeshayajua, yaliyobaki ni marudio tu)...
Kwa watu ambao ni intellectuals waliopo ndani ya jukwaa hili na pia ndani ya nchi yetu, wewe ni mmojawapo. Nimekukubali sana. Umesomea mambo ya Saikolojia, au wewe ni counsellor au daktari wa binadamu?
 
Wapumbavu wengi wako hapa... Utadhani wanalipwa.

Kila dk mbili yanapost.
 
Nimemuelewa sana huyu porofesa. Ila naona anawaweka watu kwenye denial maana "the first step towards healing is acceptance".
 
Back
Top Bottom