Ushauri wa buree kwa wote

NYAGI DRY

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2011
Posts
419
Reaction score
219
yan mi nataka niwape ushauri ndugu zangu ambao hamna kazi,kazi simpaka uajiriwe na serikali au taasis binafsi, yan kila siku utasikia au kuona watu wanasema, sina kaz niko tu nyumban, sasa basi fursa ziponying kama utajishughulisha, ona mi nlivofanya nawe waweza kuiga ka itakufaa, nlimaliza udsm b.a sociology 2011, nlikua na laptop moja nliyotaka nayochuo, nkafight nkapata desk top 2, nkaanzisha training centre , nafundisha microcomputer packages kwa mda wa wiki 2, ambapo nimepiga debe napata wanafunzi 30 mpk 40, ambapo kila kozi ni elfu 20 ,ambapo nalipa chumba nacho tumia, mwanzon nlipata changamoto, lakin kwa sasa sitak tena ajira ya mtu, hivyo basi hata mungu anasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, we kaa nyumban sema hakuna kazi udhan utaletewa hapo ! Hivyo mi nataka vijana tujitume,tutafte fursa , unaweza ukaanzisha hata twisheni centre bado ukala hela kuliko kukaa nyumbani!!
 
Wazo zuri
Lakini kumbuka kumuomba sana Mungu
ili udumu katika mazuri yenye tija.
 
Wacha hizo wewe mshukuru Mungu, kuna watu wanamaliza chuo huku hawajawahi kumili komputer kisa boom wanagawana na wadogo zake ili nao wasome,mfano mzuri ni mimi nilikuwa tena computer science lakini sikuwahi kumili computer mpaka namaliza chuo.Sasa wewe kwa kuwa umeweza si kila mtu anaweza na kumbuka wengine wakimaliza chuo wanarudi vijijini kwao ambapo hata kama ana laptop lakini umeme hakuna,wacha kubeza watu wewe mshukuru Mungu kwa maono hayo
 
 
umeongea vema!ila bado una safari ndefu sana,kufikia utakako

kitu kikubwa ni sisi vijana kutafuta fursa zilizopo hapa nchini,ili tujikomboe,tusitegemee watu fulani wakiingia madarakani watatukomboa
 
ongera sana,ni jambo la busara kumshukuru mola.
 

hauna jipya..!
 
Mnapeana mawazo mazuri lakini ni mawazo ya kuharibu....
Hii tunaita Destructive Entrepreneurship......
Unaanzisha Tuition Centre hujui hata maana ya mtaala....wewe ndio kila kitu...mwalimu wa History,Geography,Kisw,Maths,Physics,Agriculture n.k....
Unakula na kupata fedha sawa tunakubali....lakini angalia mchango wako katika kutoa daraja sufuri....angalia jinsi unavyowafanya vijana kuwa too bookish...hujui teaching methodology n.k..

Ni jambo zuri kwa kuwa nchi yetu inaenda kiholela na mambo ndio kama hayo bora kungekuwa na Tume na hivyo vituo kusajiliwa katika uanzishwaji wake.
 
Big up mjomba.Ni muhimu kupeana mawazo na kutiana moyo ili tuzishinde changamoto za kimaisha.:A S 39:
 
jARIBU KUWA NA UPEO WA KUONA MBALI SIO KAMA MWENZAKO KAANZISHA KOZI YA KOMPUTER BASI NA WEWE UFANYE HIVYO JARIBU KUFIKIRIA NJIA MBADALA HUO NI KAMA MFANO TU KWAKO!! KAMA KWELI UKO KIJIJINI SI UJIUNGE NA KILIMO KWANZA NA WEWE UTOKE:smile-big:
 
Nadhani hujamwelewa vizuri. Yeye amejitolea mfano yeye, kila mtu anapata fursa ya aina yake. Hivyo anamaanisha utumiaji mzuri wa fursa tunazopata sio kubeza ambao hawana kazi. I hope utakua umemwelewa vizuri sasa.
 
 
Centre yako imesajiliwa? au tuition centre?
 

Mbona ume panic kijana..kama nimemwelewa vzuri mtoa mada hajasema na wewe ufungue comptr centre,huo ni mfano wake yeye kutokana na mazingira aliyokuwa nayo,na wewe comptr scientst kutokana na mazngra uliyokuwa nayo changanya kichwa jinsi gani unaweza kutoka..maisha si rahisi namna hiyo kama kuandika code lazima u fight ili utoboze....kama mpaka sasa hauna kazi ebu jaribu ku team up na huyo jamaa mfanye k2 pamoja,ye anafundsha basicz alaf wewe comptr scientst ufundshe advans lke comptr maintnce na vurugu nyngne kama hzo...
 


mia mkuu naunga mkono hoja hii suala la kazi limekuwa kama national anthem
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…