Ushauri wa bure kwa wanawake na wanaume wanaochepuka.

Bernard bakari

JF-Expert Member
Mar 30, 2016
407
780
Ushauri huu sehemu nyingine ukienda hasa kwa wanasaikolojia unalipia pesa kuupata leo mtanzania mwenzangu unaupata bureeeee kabisa, gharama zako ni muda tu unaoutumia kuusoma ushauri huu.

Watu wengi wanayotabia ya kuchepuka, neno hili kuchepuka limechukua matumizi badala ya neno usaliti. Namainisha mwanaume anaweza kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mwingine ile hali anamke wake, au anampenzi wake mwenye lengo la kumwoa. Hali kadhalika vivyo vivyo kwa mwanamke.

Kwanza ifahamike kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria ya ndoa ya Tanzania, lakini pia ni kinyume cha dini zetu tunazoziamini hapa tunasema unakuwa unafanya dhambi ya uzinzi. Haifai tunamwuzi mwumba na pia tunavunja sheria ya nchi.

Lakini ushauri wangu wa leo ni kuwa chepuka kakangu, chepuka dadayangu lakini ole wako uchepuke na rafiki kipenzi wa mwenza wako. Yaan mpenzi wako akijua umekuja kufanya mapenzi na rafiki yake kipenzi amini usiamini hatokuja kukusamehe kamwe katika maisha yake yote. Naongea hivyo maana nimeshuhudia kijana mmoja alilala na rafiki wa mke wake yapata miaka sita sasa imepita mke wake bado anasononeka anasema bora angelala na mwanamke yeyote lakini si rafiki yangu. Mke wake amekuwa akiwatongoza marafiki wa mme wake lengo awe analipa kisasi kafanya hivyo mara kadhaa lakini bado ile hali haijamtoka kichwani ndipo nilipogundua kuwa ni pigo kubwa kufanya mapenzi na rafiki wa mwenza wako.

Nilivyoiona hali hii nikasema nije nitoe ushauri huu kwa wanajopu wenzangu ili kwa namna moja au nyingine inaweza saidia baadhi ya watu na ushauri huu ukawa unazunguka kichwani kila akitaka kufanya mambo kama haya akakukumbuka kidonda atakachomwachia mwenza wake hakitopona milele. BAKI NJIA KUU MICHEPUKO SI DILI.
 
Kizuri kula na nduguyo!!!! Khaaa wanaume wenyewe wachache, ila nashangaa kuna wanawake wanao zaidi ya wawili sijui wanawatoaga wapi
 
unajua huku JF kuna raha sana, watu yakitukumba ya kutukumba tunasema ni story za rafiki.

Ila nashauri wanaochukuliwa wapenzi wao wasipende ku revenge maana huwezi shindana na mwanaume kamwe,.

Kuna wakati nilitafakari mbona wanaume hawaitwi malaya wakiwa na wanawake wengi ila mwanamke ukiwa na wanaume zaidi ya mmoja unaitwa malaya.

Please wadada wa humu, tujitunze sisi na tuangalie familia zetu, meaning tuache kulipiza lengo la kukomoa tutajikuta tumejikomoa wenyewe. Pray, pray and pray. just keep on praying for your family including your hubby.

Hayo tu ila kama nimekosea nko tayari kurekebishwa.
 
Lakini huyo dada nae, hao wanaume afadhali awe hajalala nao na kuishia kuwatongoza tu. Kulala ovyo na watu sio solution ya kumkomoa mtu, sana sana by the end of the day ataishia kuumia zaidi kwa kujiachia.
Ni kweli inauma mtu wako kulala na rafiki yako wa karibu lakini ni bora kumpotezea na kum ignore.

After all, their loss, kwa mtu wa karibu yao kama ndugu kuona utupu wao.
 
Back
Top Bottom