Hakuna kitu kama hicho ... niupuuzi mkubwa huu ..mzazi unapaswa kumlea mwanao nakumpatia mahitaji yake ya msingi yatakayo muweza kumpatia msukumo wakuweza kuzifikia ndoto zake ",
Hata kama ni mzazi masikini komaa na family yako ipatie matunzo hata kama ni haba na uionyeshe upendo" watoto wakija Julia wataelewa tu kwamba mzazi wetu ni masikini lakini hakuwahi kutu telekeza alikuwa pamoja nasi katika kila hali "
Sasa kama wewe ni mzazi halafu uliikimbia family yako" na kumuacha mtoto wako akipitia tabu za maisha ", hakika haustahiki kuonewa huruma na dunia .... acha yakukute mazito
Sent using Jamii Forums mobile app
Hujielewi " ...... wewe kama una fact ongea hapa tubishane kwa hoja " kama huna ." Basi piga kimyaKweli wewe naye mtu. Bado una utoto mwingi au kichwa bongo fleva. Maana mwenye hekima na busara hawezi ongea upuuz huu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hujielewi " ...... wewe kama una fact ongea hapa tubishane kwa hoja " kama huna ." Basi piga kimya
Sent using Jamii Forums mobile app
Diamond hajawahi kukataliwa acheni fixiHujajua maumivu ya kukataliwa na mzazi wewe tena hilo neno la kumdharau futa.
Ni maumivu yasiyoelezeka wewe unazungumza tu kwa sababu ulipata malezi ya wazzi wote.
Kupewa pesa si tatizo yule mzee pesa anapata, tatizo ni msamaha ni kitu kigumu sana mwanadamu kukitoa, haihitaji media ili kupata msamaha anahitaji wasuluhishi shauri yake.
Prove it, dadavua.
Hahaa " nenda kapime mkuu ..akili yako haiko sawaHuna fact mkuu za mie kukaa na kuanza kubishana na wew. Otherwise, nikushauri maneno ya utu uzima
Sent using Jamii Forums mobile app
Well said ..indeedAngekua hana kitu msingemwambia haya, funzo kwa wanaume wote wanaotelekeza familia zao halafu mtoto anapoibuka ndio wanaanza kutafuta ukaribu nao. Mleta mada samahani nimesoma tu kichwa cha habari
Sent using Jamii Forums mobile app
Kabisa .. mzee analia ujinga ujinga" na true siatafute mali kama mwanae kwani si mwanaume piamwache mzee apande alichovuna
Simpendi diamond ... lakini kwakuwa katika maisha yangu nilichagua kuwa positive ... katika hili niko kwenye upande wake ....Mungu mwenyewe hawezi kumsamehe shetani.
Kufikia hapo mungu kanifundisha kutosamehe, roho nzuri nishaona ni udwanzi, Diamond anaufala wake ila kwenye kutomsamehe mzee wake hajakosea, haiwezekani utelekeze familia hata wanyama pori wanatunza familia zao. (mimi nimekulia nyumbani malezi ya baba na mama ningetelekezwa sijui ingekuwaje).
Namkubali Malcolm X ila baada ya kuslimu akapata akili akasema
"Ima Muslim because its a religion that teach me to respect everybody and treat everybody right and it also teach me an eye for an eye and tooth for tooth"
mambo ya kusamehe sijui staying positive in a negative situations hapana aisee.
Kwanza nikuambie siku zote Mungu hatoi laana endapo mzazi haja timiza majukumu yake na mimi nakuambia na nimeshuhudia mzazi akikupa laana au akinung'unika basi kama kweli Mzazi alitimiza majukumu yake ya malezi lazima Kuna baya litamkuta mtoto, kilio cha mzazi Mungu anakisikia sana.Naandika nikiamini kwa namna moja au nyingine ushauri huu utamfikia huyu kijana Diamond. Yeyote asiye na maelewano na wazazi/mzazi wake pia inamuhusu. Na wazazi wanaotelekeza vizazi vyao pia wanaweza kujifunza jambo.
Mimi ni mmoja kati ya watu wanaopenda namna Diamond anavyojituma katika kazi pamoja na ubunifu katika muziki na biashara ya muziki. Pia amekuwa mstari wa mbele kusaidia vijana wenzake, hususan waliotoka katika hali duni kimaisha kama ilivyokuwa kwake, kupata maendeleo kupitia sanaa. Tumeshuhudia hali kadhalika mara kadhaa akirudi maskani Tandale na kuwasaidia wakazi wa huko, kidogo alicho jaaliwa, na mengine mengi mazuri.
Yapo pia mambo kadhaa ambayo sifurahishwi nayo kuhusu yeye, lakini nitalizungumzia hili la kumtelekeza Baba yake. Nimeona mahojiano ambayo baba Diamond amefanya na online TV moja. Ni wazi kwamba huyu mzee alitibuana na demu wake Sandra - mama Diamond, akatimka nyumbani na kutelekeza familia. Anasema wakati huo Diamond alikuwa na akili yake nzuri tu, hivyo huenda Diamond aliathirika sana kisaikolojia kwa Baba yake kutokomea kusikojulikana na kuwaacha yeye na mama yake hawana hata unga robo. Kutokana na maelezo yake aliyotoa na mazingira ya nyumbani kwake, huyu mzee ana hali ngumu. Baba Diamond sasa hivi anafanya biashara ya kukopa viatu vya mtumba Ilala, anarudi kwake magomeni anaviosha na kung'arisha kisha anatembeza mtaani, yaani Mmachinga typical. Anapoumwa kwa mfano, anakuwa hana hata fedha ya matibabu, hivyo kugeuka ombaomba. Kutokana na maelezo ya Mzee mwenyewe, majirani na mdogo wake Diamond anayeishi na baba yake, Diamond kufika kwa mzee wake ni tokea yuko na Wema!
Kilichonifanya kuandika huu uzi ni kwamba Baba Diamond ameomba msamaha kwa makosa aliyoyafanya. Tena amesema kwa uchungu kabisa, kwamba hata Mwenyezi Mungu husamehe. Kwa nini , yeye asisamehewe?. Binafsi naona imefika wakati Diamond akunjue moyo wake na kumsaidia Baba yake. Katika Qur'an, ipo wazi kabisa, kwamba baada ya Mwenyezi Mungu, wanafuata wazazi. "Be grateful to Me and to your parents; to Me is the [final] destination." (Quran 31:14). Mzee Abdul alikosea kumtelekeza mtoto Diamond, haijalishi walitibuana nini na mama Diamond. Diamond hajui nini hasa kilitokea. Mzee ameomba msamaha, anapaswa kusamehewa na maisha yaendelee.
Diamond rudisha maelewano na umsaidie baba yako. Amejutia na ameomba msamaha. Kwa sasa haikupunguzii chochote kumsaidia mzee wako aishi maisha ya kawaida, ya angalau ajue familia yake itakula nini jioni. Utakuwa na amani, Itakuongezea heshima katika jamii, na zaidi utapata credit kwenye daftari lako la Akhera. Maisha yenyewe ndiyo haya. Ukiishi sana 80. Ukiishi zaidi ya 80 ni maumivu tu, uwe na hela au huna. Akifa huyu mzee katika hali hii, Diamond utaaibika Duniani na akhera.