Suala la kujua biashara gani! Linategemeana sana na Udadisi (wako mwenyewe) wa taarifa za mazingira uliyopo (fursa zilizopo).
Mazingira uliyopo yaani hali ya soko (yaani udhaifu na uimara katika bidhaa na huduma zilizopo eneo husika) katika eneo unalotaka kufanya hiyo biashara. Hii ndiyo njia rahisi ya kujua/kukushauri ni biashara gani ufanye.
Na unaposema hali ya soko inajumuisha (watu, kiwango cha huduma zilizopo,au bidhaa zinavyopatikana au kuuzwa mzunguko wa fedha, kujitoshereza kimazingira. n.k)
La sivyo kwa humu watu tutakueleza biashara ambazo, kwa mazingira yao zinalipa. na kwa mazingira yako pengine zitakuwa hazina mzunguko mzuri!
Hivyo unapoomba ushauri hakikisha unatoa na hali halisi ya eneo unalotaka kufanya biashara. kwa maelezo zaidi unaweza kun PM.