Ushauri wa biashara

Suala la kujua biashara gani! Linategemeana sana na Udadisi (wako mwenyewe) wa taarifa za mazingira uliyopo (fursa zilizopo).
Mazingira uliyopo yaani hali ya soko (yaani udhaifu na uimara katika bidhaa na huduma zilizopo eneo husika) katika eneo unalotaka kufanya hiyo biashara. Hii ndiyo njia rahisi ya kujua/kukushauri ni biashara gani ufanye.
Na unaposema hali ya soko inajumuisha (watu, kiwango cha huduma zilizopo,au bidhaa zinavyopatikana au kuuzwa mzunguko wa fedha, kujitoshereza kimazingira. n.k)

La sivyo kwa humu watu tutakueleza biashara ambazo, kwa mazingira yao zinalipa. na kwa mazingira yako pengine zitakuwa hazina mzunguko mzuri!

Hivyo unapoomba ushauri hakikisha unatoa na hali halisi ya eneo unalotaka kufanya biashara. kwa maelezo zaidi unaweza kun PM.
 
BIR kukujibu vizuri sana na kuweka msimamo wa wewe kufanya biashara. Mimi picha naomba kuongea kidogo.

Ni vizuri ukasema upo maeneo yapi ili upewe ushauri kwa kuzingatia eneo ulipo.
Msingi wa kufanya maamuzi sahihi ni kuwa na taarifa sahihi. Tafuta taarifa zinazoweza kukusaidia kufanya maamuzi sahihi.

Matatizo yanayoizunguka jamii ndio fursa ya biashara, yaangalie kwa maono tofauti.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom