Ushauri unahitajika!!!!!!

saudari

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
2,655
Reaction score
2,783
Habari zenu wana MMU, natumaini mu wazima wa afya!!!!!!!!!!!!

Leo katika pitapita zangu za hapa na pale nikakutana na mpenzi wangu wa zamani ambae tulitokea kuipendana sana,
ila tulikuja kutengana nae kwa sababu zilizokua nje ya uwezo wangu coz alichaguliwa kusomea nje ya nchi hivyo ikasababisha kutoonana kwa kipindi cha muda mrefu almost 4 years.
Tulikuwa tukiwasiliana mara kwa mara kupitia simu huku tukipeana maneno matamu ambayo yalinipa faraja nakunifanya nihisi kwamba hatuko mbali.

Siku moja alinipigia simu akaniambia kwamba kwa sasa tuishie hapo kwani hayuko tayari kuendelea kimapenzi na mimi,
Nilishindwa kumwelewa na nukiajitaidi kumuuliza je ni wapi nilipokosea lakini hakunieleza hivyo nikabaki solemba.
Nilijitaidi kumtafuta tena ili aweza kunieleza ni wapi nilipokosea lakini hakupatikana tena.

Ilinichukua muda kumsahau maana mnilitokea kumpenda sana, ila baada ya mwaka mmoja kupita nilimpata msichana mwingine ambaye aliweza kunisahaulisha matatizo yangu yote.

Hivi leo nimekutana na yule mpenzi wangu wa zamani eti anadai yuko tayari kuwa na mimi,
but mimi nilimkatalia na kumweleza kwa sasa haiwezekani kwani nimeshampata mpenzi mwingine ambae tunapendana nae na siko tayari kumwuacha.
Ila mwanamke yule hakutaka kunielewa na akasema "atafanya lolote kuhakikisha kwamba ananipata".

Swali langu kwa wana MMU,
Je uamuzi niliyouchukua ni sahihi, na vipi kuhusu kauli aliyoisema?
 
Pumbavu peleka ujinga huu fb!!.......Unataka ushauriwe nini hapo?
 
uamuzi wako ni sahihi na unatakiwa uutete kwa gharama yoyote ile, kwa jinsi ulivyojieleza hapo juu haitakiwi kurudi nyuma.
 
umeogopa kauli yake?

Uko 'weak' kwa huyo mwanamke wako wa zamani na yeye analitambua hilo
 
"atafanya lolote kuhakikisha kwamba ananipata".
hivyo ni vitisho tu endelea na msimamo wako
 
mbona vitisho sana kwenye mapenzi? na wewe mwambie utamfanyia ile mbaya
 
Unaonekana bado unampenda huyo mwanamke ndio maa huamini ulicho mwambia!

Simamia maamuzi yako kama kweli unampenda huyo msichana wako wa sasa!
 
Pumbavu peleka ujinga huu fb!!.......Unataka ushauriwe nini hapo?

Sioni sababu yakupeana maneno makali namna hii, kama huwezi kunishauri ni bora usicomment chochote.
 
umeogopa kauli yake?

Uko 'weak' kwa huyo mwanamke wako wa zamani na yeye analitambua hilo

Kauli kama hiyo sio rahisi kuivumilia kwani ukizingatia ni seriousissue.
We mtu anakuambia kauli kama hiyo ukizingatia yeye nda alisababisha muachane coz hakuweka wazi nini hasa kilichosababisha afanye hivyo.
 
"atafanya lolote kuhakikisha kwamba ananipata".
hivyo ni vitisho tu endelea na msimamo wako

Thanks for your advise.
Nadhani hayo ni maneno ya mkosaji coz ameshaona hatoambulia kitu.
 
mbona vitisho sana kwenye mapenzi? na wewe mwambie utamfanyia ile mbaya

Mi nadhani vitisho huja tu pale mtu anapoona hana tena uwezo wakukupata so anafanya hivyo ili aweze kuurudisha moyo wako nyuma.
 
saudari mwambie awasalime kigoma.....
 
Last edited by a moderator:
umeogopa kauli yake?

Uko 'weak' kwa huyo mwanamke wako wa zamani na yeye analitambua hilo

Kwa kweli alipaswa kuwa mkali na kumwambia yeye ndiye aliyesema 'sasa mimi na wewe basi'. Kwa hiyo hata majadiliano naye kuhusu uhusiano naye hayana nafasi tena. Weakness haitakiwi katika masuala ya mahusiano. Wanaoona mbele hawaambii wapenz wao 'mimi na wewe sasa basi'. Wanakauka tu na kupunguza mawasiliano.
 
Unaonekana bado unampenda huyo mwanamke ndio maa huamini ulicho mwambia!

Simamia maamuzi yako kama kweli unampenda huyo msichana wako wa sasa!

Never follow your heart in this life na hakuna mapenzi chini ya mbingu bali upo wajibu mbele za mungu, tekeleza huo. Ulitupwa ukaokotwa ukaonyeshwa utu na huo ndio upendo wa kweli na ni kwa kuzingatia matakwa ya kimungu ndipo kiasi fulani cha penzi kitakapoweza kukutembelea. Sahau kabisa kuhusu mahusiano yako ya awali na usimamapo na mungu hakuna kitisho kitakachofua dafu kwako na hakuna kitakachoenda kinyume na matarajio yako.
 

I think your right.
 
saudari Mkuu achana na huyo shetani.Samahani kwa lugha niliyotumia.Yeye alikuambia muishie hapo ukakubali, hivyo lazima aheshimu uamuzi wako wa sasa.Hivyo vitisho vya kawaida sana hakuna kitu hapo,amemwagwa huko sasa anarudi.
 
mimba iyoo ukiingia mkenge tuuuuuuuuuu............unayeeeeeeeeee
 
mimi personally nawashangaaga sana watu wanosema tulipendana sana lakini tukaja tukaa achana? umeonawapi wanaopendana wanaachana? point ya msingi ni hii wewe ulikua unampenda hlf sababu ya hisia hizo ukahisi naye anakupenda wkt sio uhalisia kama kweli angekua anakupenda asingeruhusu muachane...sijatoa ushauri lkn tafakari the chukua hatua kwa nilichosema hapo..ova...
 
Uamuzi wako ni sawa kabisa,songa mbele achana na huyo kahaba tu na wako wengi wa dizaini kama hii hapa Bongo,wanapendapenda kila mwanaume na kukosa msimamo!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…