Ushauri unahitajika tafadhali

Prince jr 47

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2016
Posts
285
Reaction score
246
Habari zenu wana jukwaa hili la MMU na wote nawatakia heri ya Mwaka Mpya wa 2017 ukawe wenye baraka tele kwenu nyote.

Back to the topic,ni hivi mimi ni member wa siku nyingi sana wa humu jf ila nimeamua kutumia hii Id yangu nyingine kuleta hili tatizo kwenu.

Mimi ni kijana wa kiume ninasoma katika chuo kikuu kimoja wapo ndani ya nchi katika mkoa fulani,nilikuwa na girlfriend wangu ambae nimedumu(au kukaa nae) katika mahusiano kwa muda wa takribani mwaka mmoja sasa....

Tatizo lenyewe ni kwamba katika mahusiano yetu tumekuwa tukipendana sana na izingatiwe kuwa mimi ndie niliemtoa usichana wake,juzi kati wakati msimu wa sikukuu unaanza yeye na familia yake waliamua kusafiri kuelekea zanzibar kwa ajili ya mapumziko ya sikukuu za krismas na mwaka mpya.

Alisafiri yeye,mama yake na mdogo wake wa kike,tatizo kuu ni kwamba tangu aende huko zanzibar amebadilika sana,amekuwa ni mtu ambae hanitafuti kabisa kwa mawasiliano kabisa,sio kama zamani nikimuuliza anasema yupo close na mama yake,nisipomtafuta kwenye simu ndo kabisa yeye hanitafuti wakati sio kawaida yake.
Kabla ya kusafiri nilimpinga sana kuhusu hiyo safari yake lakini yeye alionesha kung'ang'ania sana kwenda.

Tangu aende huko visiwani zanzibar amebadilika sana sio yule niliemjua mimi,nimemtafuta kwenye simu na kumueleza lakini ananijibu niache kulalamika yeye yupo kawaida tu,mimi hapa nilipo nina wasiwasi yawezekana kuna mtu anaemega tunda langu huko aliko na izingatiwe kwamba mpaka leo hawajarudi na huko waliko hawana ndugu hata wa kusingiziwa...maisha yao ni hotelini tu bas!
Please naombeni mnipe ushauri wakuu ninapatwa na hisia mbaya yawezekana ameshaanzishiwa ule mchezo mbaya wa 0713 ndo maana ananidharau na kuniona sifai,anasema kama vipi tuachane na sio kuanza kumfwatilia fwatilia,inaniuma sana kwa sababu ndio mwanamke wa pekee niliempenda na kuamua kutulia nae,na pia nina malengo nae.
Karibuni kwa ushauri,samahani kwa maelezo marefu na uandishi wangu mbovu.
 
Jiulize..yeye na Mama take wana mahusiano gani? Sidhani Kama kufika mbali kifikra kutasaidia kutatua tatizo ..tena ulitakiwa uwe na amani maana baby wako yuko kwenye mikono ya mama...jaribu kuwa mvumilivu.... Akirudi ongea nae na ueleze hisia zako jinsi gani hukupendezwa na kauli zake...mwambie kua Kama yuko serious na wewe hatakiwi kukujibu hivyo..then umsikilize upande wake.... Ni hayo tu. Pole
 
Shule zifunguliwe tu, maana mambo si mambo
 
Duuh pole sana, but piga moyo konde, Omba tuu Uvumilivu.
 
Hivi boyfriend inaanzia wapi kumzuia binti wa watu kusafiri na familia yake???

Pia huyo binti ni kindergaten mpaka adakwe??? Kisa wanaishi hotelini?????

Dhibiti wivu wako....mheshimu mwenzio....poa kuwa mvumilivu..... labda anaogopa mama yake atajua ana mpenzi?????

Kwa nini usivute subira mpaka arudi umhoji???
 
Huna haja ya kufikiria vibaya akirudi kutoka huko Zanzibar muangalie tabia alio nayo kama anaiendeleza na pia umwabie hukuwa unafurahishwa na majibu yake na umsikilize atacho sema....anyway labda bata limemnogea so kakusahau kwa mda![emoji23]
 
Mmeshaambiwa ukitaka wa peke yako chukua mgomba uweke ndani,

ila hawa wanaoshindaniwa barabarani tumia kwa nafasi yako,
Hiyo siyo sabuni useme unaogopa watamaliza,
. Ikirudi ni mpya kuliko ilivyoondoka.
 
Una wivu sana. Halafu acha matusi ya reja reja kwa wazanzibar. Mtu kwenda vacation kwa muda mfupi tu ushaanza hisi analiwa 071 hiyo ni dharau,unamchukulia huyo binti kama chombo cha starehe na si kama mwenza wako wa kusaidiana kwenye shida na raha.
 
I feel you mkuu
Msubiri arudi umuulize vizuri inawezekana hakuna lolote baya analofanya huko

Pole.
 
Kwahiyo akirudi utamjaribu hyo namba.!!??
 
Ukiona manyoyaaaaa...... Pole ndo maisha
 
subili akirud mkuu mbona unamkosea heshima hivo mwenzio kwamba yy hachagui jmn
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…