Habari zenu wana JF. Kuna dada mmoja hivi baada ya kufahamiana nae mwaka 2011 na kuzoeana nae na kila mmoja akijua tabia ya mwenzie nadhani alihisi kama nitamuomba mahusiano ya mapenzi baada ya kuniambia kuwa ujue wewe ni friend tu na sitarajii kama kuna siku utaniambia mambo ya mapenzi na siku ukiniambia ujue tumekosana kwakua ninae wangu nimpendae. Nilimjibu bila wasiwasi sidhani kama litatokea, na akaniambia kama huamini siku moja nitakuja kukutembelea home kwako na mpenzi wangu maana tupo free sana so hana wasiwasi na mie huyo mpenzi wangu, nikamwambia kama kweli basi karibuni sana. Kweli kuna siku alikuja nae na akanitambulisha na maisha yakaendelea kama kawaida na mahusiano ya kawaida yaliendelea. SASA KILICHOJIRI nikuwa wiki mbili zilizopita huyo dada kanipigia simu na akawa na kigugumizi katika kuongea na akawa anashindwa cha kusema nilipo mlazimisha akaniambia unamkumbuka yule mpenzi wangu ambae nilikutambulisha? Nikamwambia ndio namkumbuka kuna nini? akadai nimeachana nae kwakua nimegundua siyo muaminifu, nikamwambia basi poa. Akaniomba sana kwakua sasa yupo single nichukue hatamu maana hawezi ishi bila ya mahusiano na kwa mtu ambae amemchunguza na amempenda ndio mimi (akitiririka huyo dada). Naombeni ushauri nifanye nini maana bado mpaka sasa haelewi nipo njia gani.