Ushauri: Nina degree na nafikiria kwenda VETA nijiajiri. Kozi ipi itaniwezesha kujiajiri bila kuwa na mtaji?

Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,623
8,428
Salaam wana JF

Kama mada inavyojieleza

Mimi nimehitimu degree(Bachelor) miaka 5 iliyopita na hadi sasa nafanya kazi za kuunga unga ingawa nalipwa ila hadi mwisho wa mwezi

Nikakaa chini nikawaza nikaona niende VETA tu nikasomee fani ambayo itanifanya nijiajiri na kujipatia pesa kila siku au baada ya siku kadhaa pasipo kusubiri mwisho wa mwezi nilipwe na muajiri wangu

Fani hiyo itanifanya nijiajiri pasipo kutegemea mtaji mkubwa au bila mtaji ,yani ujuzi nitakaoupata ndio uwe mtaji wangu

Nimekaa nikawaza nikaona fani za ufundi stadi zinasaidia kwa kiasi flani kujiajiri na kuepukana na utumwa wa kuajiriwa na kusubiri mshahara mwisho wa mwezi

Sasa wadau naomba mnitajie kozi zitakazokidhi hitaji langu la kujiajiri yani nitakua napata michongo ya kufanya frequently.

Nawasilisha.
 
Rafiki yangu kulingana na hali ilivyo sasa kupata fani sio kesi kesi ni kuwa na jima mtaani ukubalike Mimi ushauri wangu wa kweli penda kufanya mile moyo umeridhia.
 
Mimi nimeajiriwa na magu lakini nilifanikiwa kusoma computer science UCC kwa lengo la kupata cheo haikuwa nilivyotarajia sasa navyoandika haya maneno nasomea Vehicle lighting na vehicle wiring kwa kuwa wewe huna kazi maalum fikiria hizi kozi ila unatakiwa uwe mjanja mjanja ili ikupe mafanikio
 
Mkuu karibi sana mm ni mkufunzi wa veta. Ningependa kujua umesomea nn degree na unaoendelea kusoma ufundi gani
 
Bachelor of tourism management, napenda kozi yoyote ya ufundi stadi itakayoniwezesha kujiajiri na kupata pesa
Mkuu karibi sana mm ni mkufunzi wa veta. Ningependa kujua umesomea nn degree na unaoendelea kusoma ufundi gani
 
Mkuu karibi sana mm ni mkufunzi wa veta. Ningependa kujua umesomea nn degree na unaoendelea kusoma ufundi gani
Mkuu,

Mimi naomba kujuzwa kuhusu kozi ya kutengeneza mashine za ofisi,
Yaani photocopy machines na printers za aina mbalimbali-

-Ipo hiyo kozi veta?
-Kama ipo, duration ni ya muda gani?
-Vilevile ada yake ni Sh. ngapi?
 
Salaam wana JF

Kama mada inavyojieleza

Mimi nimehitimu degree(Bachelor) miaka 5 iliyopita na hadi sasa nafanya kazi za kuunga unga ingawa nalipwa ila hadi mwisho wa mwezi

Nikakaa chini nikawaza nikaona niende VETA tu nikasomee fani ambayo itanifanya nijiajiri na kujipatia pesa kila siku au baada ya siku kadhaa pasipo kusubiri mwisho wa mwezi nilipwe na muajiri wangu

Fani hiyo itanifanya nijiajiri pasipo kutegemea mtaji mkubwa au bila mtaji ,yani ujuzi nitakaoupata ndio uwe mtaji wangu

Nimekaa nikawaza nikaona fani za ufundi stadi zinasaidia kwa kiasi flani kujiajiri na kuepukana na utumwa wa kuajiriwa na kusubiri mshahara mwisho wa mwezi

Sasa wadau naomba mnitajie kozi zitakazokidhi hitaji langu la kujiajiri yani nitakua napata michongo ya kufanya frequently.

Nawasilisha.
Aisee haya maisha jaribu kusomea kile unachokipenda na kukiweza na sio kile ambacho kitakupatia ajira na pesa...

Kwa ushauri...somea ushonaji wa nguo au ufundi seremala ndizo kazi ambazo hazikosi kuingiza kipato...lakkni na zenyewe zinahitaji utashi wako na juhudi.

Wapo waliosoma veta lakini bado wanasota nyumbani. Hivyo ni vizuri ukapambana na fursa za hiyo tourism management kama ulisoma kwa kupenda.

KILA LA KHERI
ASANTE
 
Mkuu,

Mimi naomba kujuzwa kuhusu kozi ya kutengeneza mashine za ofisi,
Yaani photocopy machines na printers za aina mbalimbali-

-Ipo hiyo kozi veta?
-Kama ipo, duration ni ya muda gani?
-Vilevile ada yake ni Sh. ngapi?
Hiyo kozi inafundishwa vrta changombe nenda pale kuna mwalimu mama flani hivi atakufundisha
 
Back
Top Bottom