Ushauri: Nimegundua mwanamke ninayeishi naye aliwahi kuolewa kanisani

isupilo

JF-Expert Member
Jan 25, 2015
303
1,254
Wakuu wasalam,

Naomba nisielezee historia yangu kwa sana, lakini kifupi mimi ni Mtanzania lakini katika harakati zangu za maisha niliwahi kujilipua na kukaa nje ya nchi muda mrefu.

Baadae nilirudi Bongo kama "mgeni" na kuendeleza mambo yangu. Baadae ilifika muda wa kutaka kuoa. Nilijibiidisha kutafuta mke mtanzania japo kule nilipokuwepo walikuwepo wengi ambao nilikutana nao na walipenda niwaoe.

Nilitaka kuwa na wa nyumbani. Basi nikiwa huku nyumbani nilipata mdada ambaye kwa kweli nilimpenda, alikuwa binti mzuri kwa vigezo vyangu, mtaratibu na mcha Mungu.

Mkoa tuliokutana,yeye alikuwa kikazi. Nilikaa nae kwa miaka 3 katika "uchumba". Nilifahamiana na dada zake na baadhi ya ndugu zake. Na mwisho wa siku nilikusudia kumuoa.

Kidogo nilichojifunza kwake hakuwa na haraka sana ya ndoa zaidi ya kuzaa. Wala hakuwa ananipa shinikizo la ndoa zaidi tu kuwa hata tukizaa baadae tubariki si shida.

Kwa hiyo ndugu zake walinifahamu sana, suala la kutoa mahari na kwenda kujitambulisha rasmi haikuwa mdomoni kwake. Kuna likizo moja ya week mbili niliongozana nae kwao na wazazi wake kunifahamu.

Baada ya hapo nikawa sasa kama najulikana tu; tukawa wamoja na mambo mengi ya kimaendeleo tukiwa pamoja. Mimi nikisafiri kwenda "nchini" kwangu mambo yangu namuachia na anasimamia kwa uweledi mkubwa sana.

Basi, huku na huku baadae tukapata mtoto; hapo nikiwa bado sijafunga nae ndoa iwe bomani wala madhabahuni. Ilikuwa ni baada ya kukaa nae kwa miaka mitatu.

Baadae nimekuja kugundua huyu mtu aliolewa. Tena ndoa ya kanisani haya makanisa yasiyo ya kikatoliki. Aliachana na mtu waliyeoana baada ya mwaka tu wa kuoana.

Jamaa aliyemuoa naye ana mke huko aliko na familia. Imenistua sana, kwanza nilitaka kujua kwanini alinificha, jibu likawa asingeweza kunambia sababu jamaa waliachana baada ya kuwa anadhalilishwa na kuteswa.

Sasa kuna mambo mengi yananichanganya, kwamba mpaka aliolewa na kuachika, kwanini? Halafu sasa mimi nilitaka hata kama atakuwa na mtoto lakini tubariki madhabahuni, hii itakuwaje?

Jambo hili linanichanganya sana wakuu. Mtoto wangu na kuwa na familia iliyo imara ndio ndoto zangu za kurudi kuoa nyumbani. Kama janga hili ni lako unalitatuaje?

Msaada bila dhihaka.
Asante
 
Sahau yaliyopita Mkuu kama unampenda na tayari una mtoto naye. Mnaweza kufunga ndoa hata bomani. Kama mnapendana na unaona ana vigezo vya wewe kutaka kuendelea kuwa naye basi hakuna sababu ya kumtosa. Si ajabu aliogopa kukwambia alishaolewa ndoa ya kanisani kwa kuhofia kwamba ungeingia mitini na kumuacha solemba.
 
Haina haja kufuatilia yaliyopita cha msingi je anakujali na je anastahili kuwa mke mwema kwako mengne yapo tu kumbuka kwa sisi wakirsto Kwenye Bible pameandika tusishikamane na wenye Dhambi huwez Jua je huyo mwanaume ana matatizo Gani mpaka aka achana na huyo mwanamke unajua tunafikira mbaya kwamba siku zote wabaya ni wanawake tu Bila kusahau hata wanaume nasisi sio wema kwa ushauri wangu achana na yaliyopita songa Mbele
 
madhabahu za bongo zitakuwekea vizingiti ila za nje waweza funga bila shida hasa huko uliko jilipua.kibiblia hapo ndoa hakuna huyo Dada anazini na mume wake wa awali vivyo hivyo.
ushauri kwakuwa dini wote hamuifuati kikamilifu.mnaweza oana kimila/bomani huku mkiomba rehema za Mungu namna ya kufika madhabahuni.
 
Daa!! Toka huko isupilo porini nenda pale boman mkafunge ndoa...,, kama unampenda na kwa ajiri ya mtt wenu...

lakin kwann alikuficha?
Naamin angekuambia tangu awali pengine ungejua uamueje.....

~Maisha yana mengi asee~
 
Hizo ni formality tu wala hazina mashiko yoyote. Kama mmependana sioni kikwazo hapo.. Unaweza kupata ambaye hakuwahi kuolewa lakini akawa tayar amechezewa vya kutosha.. .. So mimi kama Naantombe sione ubaya wowote hapo kwa huyo mke wako labda kama umeanza kumchoka
 
madhabahu za bongo zinaweza vizingiti ila za nje waweza funga bila shida hasa huko ulilo jilipua.kibiblia hapo ndoa hakuna huyo Dada anazini na mume wake wa awali vivyo hivyo.
ushauri kwakuwa dini wote hamuifuati kikamilifu.mnaweza oana kimila/bomani huku mkiomba rehema za Mungu namna ya kufika madhabahuni.

Haaaaa haaaa, Madhabahu za Bongo zinayeyusha, mara asivae shela, mara asisimame madhabahuni, mara mafundisho miezi mitatu, mara lazima alipe zaka, mara lazima awe anahudhuria Jumuiya nk
Sio kwamba Bongo ndio wanafata misingi sahihi ya Ukristo?
 
mara kama mmezaa hakuna shera/wala kufika madhabahuni!
 
Sahau yaliyopita Mkuu kama unampenda na tayari una mtoto naye. Mnaweza kufunga ndoa hata bomani. Kama mnapendana na unaona ana vigezo vya wewe kutaka kuendelea kuwa naye basi hakuna sababu ya kumtosa. Si ajabu aliogopa kukwambia alishaolewa ndoa ya kanisani kwa kuhofia kwamba ungeingia mitini na kumuacha solemba.
Asante kwa hekima zako!!Hili jambo linanichanganya sana mkuu.

Nimekulia kwenye dini,hata kama nina mapungufu kama binadamu,lkn suala la ndoa nilitaka lifanyike madhabahuni...Kusema kumuacha wakati kuna mtoto,ni kusababisha mtoto akikua aone kama mimi baba nina makosa

Nilipenda kuwa na watoto wa "baba na mama mmoja"
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Historia ndio inatoa picha. Je wewe ni Kristo? Mama ndio naenda kwa mchungaji akushauli. Sip hapa ! Walioshindwa wote wanakwambia usitazame historia! Ata wewe umeanza Eliza historia kwanza.
 
Hapo ni pagumu Mkuu lakini hata Mungu atakuelewa kama ndoa yako haifanyika madhabahuni. Hapa unalinda familia yako kuendelea kuwa pamoja. Unaweza kuamua kuoa mwingine halafu akawa pasua kichwa ukabaki kujuta tu Mkuu.

Asante kwa hekima zako!!Hili jambo linanichanganya sana mkuu.

Nimekulia kwenye dini,hata kama nina mapungufu kama binadamu,lkn suala la ndoa nilitaka lifanyike madhabahuni...Kusema kumuacha wakati kuna mtoto,ni kusababisha mtoto akikua aone kama mimi baba nina makosa

Nilipenda kuwa na watoto wa "baba na mama mmoja"
 
Haina haja kufuatilia yaliyopita cha msingi je anakujali na je anastahili kuwa mke mwema kwako mengne yapo tu kumbuka kwa sisi wakirsto Kwenye Bible pameandika tusishikamane na wenye Dhambi huwez Jua je huyo mwanaume ana matatizo Gani mpaka aka achana na huyo mwanamke unajua tunafikira mbaya kwamba siku zote wabaya ni wanawake tu Bila kusahau hata wanaume nasisi sio wema kwa ushauri wangu achana na yaliyopita songa Mbele
Na hili jambo la mimi kugundua limempa shida sana,amedhoofu na hana amani tena.Anahisi wakati wowote nabwaga manyanga.

Nampenda sana mwanangu...Dhamira inanisuta kumfanya aje akae na Mama bila baba...Lkn misingi ya imani za dini nazo zinanifunga!!Nifanye maamuzi gani?ndio nilipo njia panda
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hapo ni pagumu Mkuu lakini hata Mungu atakuelewa kama ndoa yako haifanyika madhabahuni. Hapa unalinda familia yako kuendelea kuwa pamoja. Unaweza kuamua kuoa mwingine halafu akawa pasua kichwa ukabaki kujuta tu Mkuu.
Mungu anisaidie...Dunia na majaribu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwasasa mume wake ni kama mshitaki wako... Kwahiyo nakushauri umtafte mpatane kwanza ndio uendelee na taratibu zingine.

Moreover si mbaya ukitafta ushauri kwa mchungaji wako maana hapo unaoa mke wa mtu ati shehe
 
Historia ndio inatoa picha. Je wewe ni Kristo? Mama ndio naenda kwa mchungaji akushauli. Sip hapa ! Walioshindwa wote wanakwambia usitazame historia! Ata wewe umeanza Eliza historia kwanza.
Sijakuelewa...japo naweza kusema jukwaa hili lina viongozi pia hata wa dini na watu wenye ufahamu
Tunahimizwa tusikae na mambo kifuani...Kabla sijaenda kanisani kupata ushauri wa kiroho,naweza kuanza kwa ndugu jamaa na marafiki.

JF ni sehemu kati ya hizo.Mjumuiko wa ushauri ndio utanipa mwanga wa kutoka sehemu moja kwenda nyingine.Kwa hiyo,kwangu JF bado ni sehemu sahihi ya kuanza kwa ushauri.

Hapa kuna uhuru wa kujieleza na kuelezwa sbb hatujuani na kuoneana aibu
 
Kila la heri Mkuu. Unaweza kuruka mkojo ukaishia kukanyaga kinyesi na kubaki na majuto mjukuu. Kama huyu ana vigezo vya kustahili kuwa mkeo na mama wa watoto wako sioni kwanini uachane naye. Ni kweli alikosea kukwambia kwamba aliwahi kuolewa lakini sababu iko wazi kabisa ya yeye kuamua kutosema na pia unajua sababu ya ndoa yake kudumu kwa mwaka tu.

Mungu anisaidie...Dunia na majaribu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom