Ushauri: Nataka kufunga pingu za maisha, ila nashindwa kufanya uchaguzi sahihi

man of the year

JF-Expert Member
Jun 23, 2014
345
85
Habari zenu,

Wanajukwaa natumaini mnaendelea na majukumu ya kila siku, nimeona sio vibaya tukipeana ushauri kwa jambo nalopitia kwa sasa ingawa inaweza onekana jambo la kawaida kwa wenzangu.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 29 baada ya kuona umri unasonga nipo ktk mikakati ya kupata jiko kwa undani ni kijana mkimya sana hii imepelekea kupata sifa toka kwa majirani wanaonizunguka imefikia mahali wanataka kujua nipo na nani kwa sasa.

Naitaji kufunga pingu za maisha imekua ngumu kufanya uchaguzi uliosahihi sababu shemeji yangu(mke wa kaka) anatak nimchumbie mdogo wake amekua akitumia nguvu nyingi karibu ukoo mzima unafahamu hili.

Yupo pia binti nilie mfundisha mapenzi baada ya kupotezana muda mrefu tulipokutana akanikumbushia yote niliomhaid miaka 10 oliopita nafsi ilinisuta maana ni story ndefu.

Pia kuna huyu tumesota wote chuo na baada ya chuo nifanye uchaguzi gani hapa nisisononeshe yeyote kumbukeni nimeumbwa na huruma sana

Naombeni msaada utakaonipa ujasiri.

Asante

Nawasilisha
 
Sema na moyo wako,ndoa haipo kwa ajili ya kumfurahisha mtu ndugu bali ni mustakabali wa maisha yako.
 
wewe binafsi unampenda yupi kati yao, muoe huyo, hao wemgine hata wakiumia haitachukua miaka, act like a MAN
 
Ungekuwa na huruma huyo unayedai ulimfundisha mapenzi usingemuacha, usioe kwa sababu ya kufurahisha mtu au kulipa fadhira, Oa kwa sababu umepata mtu sahihi katika maisha yako kumbuka ndoa ndo inamalizia sehem yako ya maisha iliyobaki dunian ukikosea mwisho wake utakuwa mbaya
 
oa unaempenda wewe na sio suala la kuona huruma hasa kwa jambo la ndoa....huruma itakuponza shaur yako bora lawama kuliko fedhea.
 
Kwani shemeji yako amekushauri kila kitu maishani au wamekulea na kaka?

Kwanini ujiulize mapenzi ya kulazimishwa sio mazuri na inaelekea upo zaidi kwa wa tangu enzi haya elekea huko.

Huyo shem akikupiga mkwala msingizie anachepuka arakuheshimu nunua simu kadi ingine tuma maujumbe machafu vizia kaka hazikamate au mtumie ujumbe muite kaka wa jina la shem unataka msalimu na wewe ni bwana ake.

Aaaagh
 
Habari zenu,

Wanajukwaa natumaini mnaendelea na majukumu ya kila siku, nimeona sio vibaya tukipeana ushauri kwa jambo nalopitia kwa sasa ingawa inaweza onekana jambo la kawaida kwa wenzangu.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 29 baada ya kuona umri unasonga nipo ktk mikakati ya kupata jiko kwa undani ni kijana mkimya sana hii imepelekea kupata sifa toka kwa majirani wanaonizunguka imefikia mahali wanataka kujua nipo na nani kwa sasa.

Naitaji kufunga pingu za maisha imekua ngumu kufanya uchaguzi uliosahihi sababu shemeji yangu(mke wa kaka) anatak nimchumbie mdogo wake amekua akitumia nguvu nyingi karibu ukoo mzima unafahamu hili.

Yupo pia binti nilie mfundisha mapenzi baada ya kupotezana muda mrefu tulipokutana akanikumbushia yote niliomhaid miaka 10 oliopita nafsi ilinisuta maana ni story ndefu.

Pia kuna huyu tumesota wote chuo na baada ya chuo nifanye uchaguzi gani hapa nisisononeshe yeyote kumbukeni nimeumbwa na huruma sana

Naombeni msaada utakaonipa ujasiri.

Asante

Nawasilisha
Moyo wako umempenda yupi? kama mtu hafai ni janga lako mwenyewe.
wewe ndio utakayeishi na huyo mwanamke
 
maisha utakayoenda kuishi ni ya kwako hakuna atakayekusaidia.
usioe kwaajili ya kumuonea mtu huruma, au woga wa shemeji yako, oa mtu unayeona moyo wako una amani nae na utakuwa na furaha.
 
Back
Top Bottom