Ushauri: Nassari achana na siasa za Godbless Lema

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Ninaamini wewe ni kijana unayejitambua na pale unapotambua makosa yako huwa unajaribu kujirekebisha.

Huna elimu ya ‘’hapa na pale’’ yenye vyeti vya ‘’hapa na pale’’ kama Godbless Lema au Saed Kubenea. Elimu yako na vyeti vyako vinajulikana na kuheshimika kitaifa na kimataifa.

Umelelewa na kukulia katika familia yenye maadili ambayo inamuogopa Mungu. Wazazi wako ni Wachungaji katika Kanisa.

Kama uliweza kukataa usanii wa kisiasa wa Lema, unatakiwa kukataa pia mitindo yake ya kilaghai kwa wananchi.

Achana na siasa nyepesi kama za Lema za kupiga picha ukiangalia vifaa/vitanda vya hospitali nje ya nchi na kuweka picha kwenye public domain ili kupata cheap populality.

Kumbuka Lema alienda Uingereza kupiga picha za Helikopta na gari za wagonjwa halafu akatueleza amekwenda kununua kwa ajili ya wananchi wake wa Jimbo la Arusha.

Mpaka sasa kwa miaka zaidi ya minne vifaa hivyo hatujaviona na hataki tena kugusia suala hilo kwa wananchi wa Jimbo la Arusha. Kwa lugha nyingine, alifanya siasa za kisanii zenye matunda ya muda mfupi.

Kwa habari zaidi unaweza kusoma thread hii;

Nassari endelea na kazi ya kuwatembelea wananchi wako na kujibu matatizo yao kivitendo kama uliovyofanya katika hospitali ya Tengeru. Achana na cheap political attention with empty vessels as you may know, empty vessels make most noise!

lema-chopper.jpg

Godbless Lema akiangalia moja ya Helikopta alizodai kununua kwa ajili ya kazi zake kama kiongozi wa CHADEMA.
600.jpg

Gari za kubebea wagonjwa ambazo zilidaiwa kupewa na wanachama wa Tawi la CHADEMA, Uingereza kama moja ya ahadi kwa wananchi.
=================================================================
Joshua Nassari akiwa nchini China kununua vifaa vya kusaidia katika hospitali za Meru

img-20160111-wa0007-jpg.316252
 
Msemaji Ukweli mbona ulifanya sanaa ya kukataa posho ukasema ziweke kwenye Akaunti ya NGO yako na hazikuwekwa zikaendelea kuwekwa kwenye Akaunti yako na hukuzirudisha , huo sio usanii? Ukitaka kukosoa jitazame kwanza .........
 
Naona amekosa la kusema.Nasari mdogo Fanya kadiri ya uwezo wako
 
Lengo lako ni kumsema Mhe. Gobless Jonathan Lema na wala sio kumshauri Nassari. Ila ujue Lema ameshaileta hio Ambulance Arusha na sasa anajenga hospitali ya Mama na Mtoto-MCH. Pia jambo KUBWA alilofanya kwa wana Arusha ni KUWAJENGEA MIOYO YA UJASIRI na kutetea haki zao. Woga ni DHAMBI. Mhe. Gobless Jonathan Lema (MB) Arusha Mjini HACHAFULIWI KWA MANENO YAKO YA KWENYE KHANGA. Habari ndio hio...
 
Msemaji Ukweli mbona ulifanya sanaa ya kukataa posho ukasema ziweke kwenye Akaunti ya NGO yako na hazikuwekwa zikaendelea kuwekwa kwenye Akaunti yako na hukuzirudisha , huo sio usanii? Ukitaka kukosoa jitazame kwanza .........
Tatizo lako ni kudhani unanifahamu wakati hunifahamu!

Jaribu kwanza kutatua tatizo lako la kudhani unanifahamu ili upate msingi bora wa kuchanganua na kujenga hoja!
 
Tatizo lako ni kudhani unanifahamu wakati hunifahamu!

Jaribu kwanza kutatua tatizo lako la kudhani unanifahamu ili upate msingi bora wa kuchanganua na kujenga hoja!
Mbona umekurupuka kama Ngiri ? Unafikiri IPI zinadanganya sio ? list ya walioficha mabilioni Uswisi iko wapi ? au nalo lilikuwa ni unafiki?
 
Fisiemu utawajua tu hapa ni uchonganishi wako ili ufikishe ujumbe kwa lema. Ujumbe umewafikia ila mbona juzi tu ndo wamenurudisha mjengoni kwa mbwebwe zote?
Hukuona ilibidi uongozi wote wa CHADEMA, Lowassa na genge lake walipiga kambi katika Jimbo la Arusha Mjini ili kufanya kampeni wakati Nassari hakuhitaji nguvu hiyo katika Jimbo lake kwa sababu hakuwahi kutanguliza ulaghai katika kuwatumikia wananchi wake.
 
Kama Lushoto kambi ilivyoweka na ACT na kuambulia kura mamia .......teheh.....
 
Lengo lako ni kumsema Mhe. Gobless Jonathan Lema na wala sio kumshauri Nassari. Ila ujue Lema ameshaileta hio Ambulance Arusha na sasa anajenga hospitali ya Mama na Mtoto-MCH. Pia jambo KUBWA alilofanya kwa wana Arusha ni KUWAJENGEA MIOYO YA UJASIRI na kutetea haki zao. Woga ni DHAMBI. Mhe. Gobless Jonathan Lema (MB) Arusha Mjini HACHAFULIWI KWA MANENO YAKO YA KWENYE KHANGA. Habari ndio hio...
Sidhani kama umeelewa hata ulichokiandika!

Kama utakuwa umekielewa ulichokiandika, basi utakuwa una matatizo makubwa sana kifikra!
 
Sidhani kama umeelewa hata ulichokiandika!

Kama utakuwa umekielewa ulichokiandika, basi utakuwa una matatizo makubwa sana kifikra!

Kila anaye comment ANAKUKOSOA WEWE. Lazima UNA MATATIZO makubwa ya AKILI, Nimeshakupuuza
 
Hukuona ilibidi uongozi wote wa CHADEMA, Lowassa na genge lake walipiga kambi katika Jimbo la Arusha Mjini ili kufanya kampeni wakati Nassari hakuhitaji nguvu hiyo katika Jimbo lake kwa sababu hakuwahi kutanguliza ulaghai katika kuwatumikia wananchi wake.
hata huyo nassari ni wa chadema sio wa ugambani, hongera kwa kusifia makamanda wa chadema
 
Hoja utumbo?
Ingekuwa ni hoja utumbo nadhani usingepoteza muda wako na kuumiza vidole vyako kutoa mchango wa kitoto!

Inawezekana hijitambui na kwa maana hiyo, huwezi hata kutambua na kuelewa kimantiki kile ambacho unakifanya kwenye thread!
 
Mbona unajazba sana mkuu , Hapo Lumumba yaelekea jua Kali sana ndo mana Kila kukicha unamfatilia lema Hebu mwache mbunge wetu . Alichokifanya arusha tunakijua wenyewe .
 
Mbona huulizi ulaghai wa walosema Tanzania ya Magufuli ni ya viwanda wakati hakuna umeme, elimu bure wakati watoto wanasinzia darasani kwa njaa,milioni hamsini kila kijiji huku hakuna hata dalili ya kupata milioni moja!
 
Back
Top Bottom