Kuna rafiki yangu yupo katika mahusiano takriban miaka 4 sahivi, na toka waanze uhusiano na huyo kaka, walipendana sanaaa yaani na huyo rafik yangu siyo mtu mwenye tamaa ya hela kitu ambacho wasichana wengi wa siku hizi wanaangalia sana.
Alikuwa anamsaidia huyo kaka hata akiwa na shida ya hela lakini siku hizi huyo rafiki yake wa kiume ameonekana kubadilika sana kwani hata akipiga simu atamwambia subiri halafu hampigii tena au hata wakiwa wanaongea kwenye simu anamkatia bila sababu na wala hasemi na hamtafuti. Akimtumia sms hazijibiwi yaani ameonekana kubadilika tofauti na alivokuwa mwanzo.
Ameniomba ushauri afanyaje nami nmeona ni vema nilete uzi huu kwenu wana JF tumsaidie ushauri huyu rafiki yangu maana binti anampenda sana na ndugu zake huyo kaka wanamfahamu na wanampenda sana huyo dada ila huyo kaka ndo tatizo afanyaje.
Karibuni sana.
Mdada, mpe pole yake, hicho kinacho mpata mm nina true story yake, rafiki yangu kabisa true best frd, alikuwa na msichana, huyo mdada si haba mambo safi, wameenda kipindi kirefu mpka yule dada akaamua kumsimesha best angu chuo furani cha ualim
Mdada alikuwa anatoa service zote unazozijua za kijamii kwa ndugu na jamaa wa hyo best angu, kunasiku nlikuwa nataka kwenda kumuona hyo best chuon, yule mdada alinitoa mkoa wangu(dar)mpaka musoma alikokuwa anasoma best wangu,
Nlipofika nkamkuta yupo na mrembo mwingine, nlipo muuliza y, akaniambia yule anae tu ila hamfurahii,
To short a story, dada aliachwa na jamaa sasa anamke mwingine, nlichojifunza ni kuwa ukimuona mkaka anaanza mabadiliko na kama ulikuwa unatoa service kuwa makini maana hakika utaachwa tu, havutiwi nawe ila anavutiwa na pesa,
Mwambie ajiandae kisaikolojia ndo amekwisha achwa hivyo, hakina namna...