atlas copco
JF-Expert Member
- Jun 15, 2015
- 8,463
- 9,667
Nina mpenzi wangu ambaye tumekuwa ote toka nikiwa shule ya msingi mpaka saivi nimefika Chuo Kikuu nasoma hapa Chuo Kikuu cha mtakatifu Augustine (SAUT) Tawi la Mwanza mwaka wa Pili.
Nimekuwa nae kwa Muda mrefu sana katika shida na raha na mpenzi wangu amenisaidia mambo mengi sana japokuwa hana kazi anauza mitumba lakini amenisaidia sana nakumbuka nikiwa form six yeye ndo aligharamia ada na kila kitu wazazi wangu hawakutoa hata shiling tano na wakati nakuja Chuo Kikuu Hapa yeye ndo alinipa nusu ya ada yangu wazazi walimalizia nusu, kwa kweli namshukuru sana maana bila yeye pengine nisingekuja hata kuanza masomo first year maana wazazi wakati ule natakiwa kuja chuoni walikuwa na hali mbaya kifedha lakini yeye mpenzi wangu alinisaidia mpaka nikafika kureport chuoni na kuanza masomo.
Wakati namalizia first year, niliumwa ghafla na nilipoenda hospital madaktari wakaniambia Figo zangu zote zimeharibika na nisipofanya haraka kuzibadilisha nitakufa, wazazi wangu walihangaika sana kutafuta mtu wa kuniwekea Figo lakini hakupatikana.
Baadae mpenzi ambaye wazazi walikuwa hawamfahamu kwa sababu tulikuwa wapenzi tu akaamua kujitolea Figo Moja na yeye abaki na moja na madaktari walipompima wakaona Figo iko salama wakamfanyia upasuaji na kutoa figo moja ikawekwa kwangu moja akabaki nayo yeye na nimepona wote tuko salama. Sasa wakati naanza Mwaka wa Pili nilionana na kijana mmoja Handsome kweli ameumbika hakuna mwanamke anaweza kumkataa kwa uzuri wake Sasa alitokea kunipenda sana.
Alinitongoza nikamkatalia lakini kadri alivozidi kunibembeleza taratibu na mimi nimejikuta nimevutiwa nae sana kwa sababu amekua karibu na mimi sana hapa Chuoni mpaka nimeanza kumsahau mpenzi wangu na kwa vile niko nae mbali nimejikuta namsahau na najikuta sina hamu nae kabisa na sio siri nimetokea kumpenda sana huyu kijana mcheshi na muda wote huwa ananifanya niwe na furaha na kwa sasa nimeshaanzisha nae mahusiano naye kwa siri.
Nashindwa nifanyeje kwa kweli
NAJUA WENGI MTANISHANGAA LAKINI MIMI NAOMBENI USHAURI NIFANYEJE MPENZI WANGU WA ZAMANI YULE KAPUKU ANANIPIGIA SANA SIMU KUNA WAKATI NAMKATIA SIMU NA SINA HAMU NAE KABISA KWA SASA, NIMEJIKUTA SIMPENDI KABISA NISAIDIENI NIFANYEJE.
SHARE NA WENZAKO WAMSHAURI DADA HUYU.