Mleta mada unachanganya mambo, kwanza kabisa huko unakokuelezea si kutawadha. Huko kunaitwa kustanji. Kutawadha ni "process" nyingine kabisa.
Nakushauri uchukuwe kitabu chenye "hukumu za kustanji" utapata faida kubwa.
Kwa ufupi, yeyote aendae haja kubwa anatakiwa ahakikishe anajisafisha mpaka ule "ulaini" unapotea na hauhisi kabisa. Ni vyema akianza kwa "toilet paper" akamalizia kwa maji kama ana matatizo.
Pia inawezekana ana tatizo la kiafya nashauri akishaelewa kustanji sawa sawa na kama hali inaendelea amuone daktari.