harder king
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 3,970
- 6,903
Habarini wana JF,
Mimi ni kijana mwenye umri chini ya miaka 30, ninaishi na mke wangu kwa kipindi kisichozidi miaka minne na tumejaliwa mtoto mmoja.
Tangu niwe na mwenzangu tumekua tukitofautiana kwa mambo mengi kwani mwenzangu amekua sio mtu wa kupenda kusahihishwa pale anapofanya kosa lolote japo mimi nimekua nikishuka na kukiri kosa pale inapotokea nimekosa. Ilifikia mahali ilibidi tuwashirikishe ndugu wa pande zote lakini hilo halikusaidia maana ilikua kila wakija wakiondoka tu tatizo linaongezeka.
Kiukweli mke wangu sio kwamba nilimpenda tu ila kutokana na maisha niliyokuwa naishi kabla nilitegemea awe mtu wa kunitia moyo na kufanya tuishi maisha ya furaha.
Sijajua sababu ni nini kwani wakati tunaanza maisha alinikuta sijihusishi na starehe ya aina yeyote. Yaani hata marafiki wasio na mawazo ya maisha sikuwa nao zaidi ya kudili na mishe zangu za kuniongezea kipato. Lakini mda mfupi tu tangu tuanze kuishi pamoja nilijikuta naanza kujiingiza kwenye ulevi tena uliopitiliza.
Nilikuwa sijawahi tamani mwanamke mwingine zaidi yake, mbaya zaidi nlianza kutamani wanawake wengine. Mke wangu hakuzipenda zile tabia ila alishindwa kuelewa nini chanzo cha yote.
Kwa upande wangu nilihisi chanzo cha mimi kuwa hivyo ni tabia zake ambazo sikuzipenda kwa kweli. Kuna wakati alifanya kitendo ambacho nisingependa kukielezea hapa hadi ilibidi vyombo vya sheria vihusishwe.
Kwa sasa nahisi kukata tamaa hadi natamani kuanzisha mahusiano mapya mbali na yeye, kwakuwa ni muda sasa tupo pamoja japo amekua na watu wanaomshauri lakini hubadilika kwa muda tu lakini ikitokea kuna kitu hakipo sawa nikiuliza kwanini hatotaka kutoa sababu zaidi ya kunijia juu au kununa siku nzima.
NAOMBENI USHAURI WENU,NIENDELEE NA MKE WANGU WA SASA AU NIKIPI NIFANYE?