Ushauri Master Degree Programme

von tosy

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2014
Posts
251
Reaction score
156
Mimi ni mhitimu wa Bach. Of Arts In Geography and Environmental Studies (Ba,GE's) kutoka chuo kikuu cha Dodoma 2016.

Baada ya kumaliza Degree yangu ya kwanza natamani kujiendeleza zaidi kimasomo ili kuweza kuongeza maarifa pia na ujuzi katika fani niliyosomea. Lengo la Uzi Huu ni kuomba ushauri Kwa watu waliopo katika fani mbalimbali kuhusiana na maswala ya soko la ajira katika degree programme zifuatazo

Master of Disaster Risk Management (M.DRM) kutoka chuo kikuu cha Ardhi

Master Degree in Environmental Planning and Management (MEP) kutoka chuo cha mipango Dodoma

Master of Science In Environmental Management (MSc.EM) kutoka chuo kikuu cha Mzumbe

Master of Arts in Geography and Management (MA GEM) kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Nitangulize shukrani Kwa wale wote watakaokua tayari kuchangia Uzi huu Kwa lengo la kuelimisha na kutoa uzoefu walionao katika fani ya tasnia husika (Mazingira na Majanga).
Naimani Uzi huu utakua msaada mkubwa kwangu na Kwa vijana wengine wenye mlengo unaofanana na wangu.

Nawasilisha.
 
Dogo katafute hela hicho ulichosomea hujaanza kukitumia..
Hii nchi imebadilika asiye na vyeti ni RC, wewe na Degree ulipaswa kuwa Rais kama kungekuwa na usawa
 
Dogo katafute hela hicho ulichosomea hujaanza kukitumia..
Hii nchi imebadilika asiye na vyeti ni RC, wewe na Degree ulipaswa kuwa Rais kama kungekuwa na usawa
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji4]
 
Dogo katafute hela hicho ulichosomea hujaanza kukitumia..
Hii nchi imebadilika asiye na vyeti ni RC, wewe na Degree ulipaswa kuwa Rais kama kungekuwa na usawa
Sawa Braza nimekuelewa
Lakini je kama nikitaka kusoma kati ya hizo Ipi iko marketable
 
Sawa Braza nimekuelewa
Lakini je kama nikitaka kusoma kati ya hizo Ipi iko marketable
Soko la ajira ni gumu sana kwa sasa, ningekuwa na muda ningekueleza kwa nini nakwambia hivyo.

Hiyo masters unayofanya ningekushauri 13M utakazotumia chimba kisima fanya kilimo cha umwagiliaji.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…