el nino
JF-Expert Member
- Nov 5, 2013
- 4,712
- 5,064
Nianze kwa kuwafahamisha ambao hawajajua pesa zao za kwenye simu huwa zinaenda wapi pindi line zao za simu zinapopotea au kutotumika kwa muda mrefu.
Ni kwamba unapoacha kutumia line yako ndani ya siku 270 na umehifadhi pesa kwenye Tigo pesa,M-pesa au Airtel Money hizo pesa zinapelekwa kwenye account maalum ya B.O.T ambapo zinakaa kwa miaka 5 kabla ya kupelekwa kwa msajili wa hazina na huko zikikaa miaka 15 serikali inazitumia, hiyo ni kwa mujibu wa sheria (Unclaimed Property Act na Financial transactions Act).
Ushauri.
Sote tunajua usiri uliopo kwenye miamala ya kifedha hasa tunapotumia simu zetu, kusema ukweli utaratibu wa ufuatiliaji uliopo ni mgumu sana utasababisha watu wapoteze fedha nyingi sana na haki zao za msingi kama haki ya urithi.
Nashauri kuwe na mfumo kwa kila anayetumia miamala ya kifedha kama Tigo Pesa na nyinginezo asiwe na namba zake maalum ambazo fedha zitatumwa huko akiacha kutumia line ndani ya hizo siku 270!!
Kwa mfano mi ninatumia Airtel Money, naingiza namba yangu moja au zaidi ambapo ntakapoacha kutumia line yangu muda mrefu pesa zitumwe huko ili kuepuka usumbufu wa hela kutumwa B.O.T uanze kwenda kwenye Kampuni ya Simu wakwambie wameuza line yako na usumbufu mwingine.
Kingine itasaidia hata haki ya kurithi, mfano mimi nikitumia M-pesa siku nikipoteza maisha haitakuwa na haja ya kuja na mabarua ya mirathi na vithibitisho vingine kuja kutaka hela ambayo hawajui hata ni shilingi ngapi ipo kwenye simu, badala yake pesa zilizopo kwenye simu zitaenda moja kwa moja kwa mtu au watu ambao ningependa fedha zielekee huko pindi line yangu itakapoacha kutumika.
Vile vile tunafahamu wengi wetu tuna line zaidi ya moja hivyo unaweza ukaacha kutumia line moja kwa muda mrefu lakini kabla hawajauza namba yako pesa zako zinaenda kwenye namba yako au namba uliyotaka iende, kuna wale wengine wanaibiwa line na wanashindwa kurenew line kwa sababu mbalimbali wataweza kupata pesa zao kwa mfumo huu.
Mi nafikiri kampuni za simu zinapaswa kuja na njia mbalimbali ambazo zitalinda na kukuza uaminifu baina yao na wateja maana wanashika pesa nyingi sana za watu hivyo serikali na vyombo vyake lazima ziangalie sheria hizi zilizopo zisije zikawa ndio kichaka cha upigaji wa fedha badala ya kuokoa fedha.