DBC
Member
- Oct 26, 2018
- 19
- 11
Kwako brother Innocent Bash (W) Viwanda na Biashara
Nikupongeze kwa uteuzi wa kushika wizara hiyo nyeti hasa ukizingatia umuhimu wake kwa maendeleo ya nchi yetu.
Karibu katika majukumu mapya kutoka kuwa Naibu waziri Kilimo na sasa Waziri VB, naomba nikupe mambo mawili matatu ya kuyarejea na ikiwezekana kuyachukua kama ushauri kutoka kwangu ili kuendelea kusukuma gurudumu la maendeleo.
1. Wizara hii ya viwanda na biashara inajumuisha majukumu mengi sana ya kiutendaji na usimamizi hivyo hupaswi kukaa ofisini kusubiri taarifa bali kila siku unapaswa kuwa eneo la tukio (field) na kufuatilia.
2. Wizara yako inahusisha biashara hivyo unajukumu la kusimamia mamlaka nyingine zote zinazowahusu wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo mamlaka hizo ni pamoja na TANTRADE, TRA, Mabenki, mamlaka nyingine za utoaji leseni na usimamizi wa viwanda.
3. Ufufuaji wa viwanda vilivyofungwa, vilivyopunguza wafanyakazi na vinavyoanzishwa viongeze uzalishaji hii ni kazi ambayo utatakiwa kuisimamia, kumbuka hii ndio inaongoza sera ya Serikali awamu ya tano, hivyo utapaswa kujikita katika kuibua, kuinua na kukuza sekta ya viwanda, nikushauri kitu katika jukumu hili la viwanda andaa muongozo wa kusaidia wawekezaji na taasisi zitakazopenda kuanzisha viwanda zipate unafuu wa kuanzisha viwanda.
4. Kuishauri mamlaka ya mapato Tanzania TRA kufuatilia taarifa za kodi kwa wateja wakubwa badala ya kukaa ofisini kusubiri wafuatwe wawafuate wao, wasimamie sheria na kanuni za mlipa kodi na sio kutumika kuwaondoa wengine sokoni na kuawabakiza wengine kuwe na uwanja sawa kwa walipa kodi wakubwa, TRA iendelee kuimarisha vituo vya kikodi vya mipakani na vile vya pamoja (One Stop Boder Post) viwe na mfumo wa Teknoljia ulioimara, walipa kodi wa kati wanaotumia mashine za EFDs pamoja na wenye vituo vya mafuta wanaotumia mashine wamekuwa na malalamiko ya muda mrefu wasilkilizwe, wafanyabiashara wadogo wawndelee kutengenezewa mazingira ya ulipa kodi kwa urafiki na TRA na sio kama shuruti ili kuwafanya waone kodi ni wajibu.
5. Andaa kongamano kubwa la wafanyabiashara kwa kushirikiana na balozi zetu zilizoko ukanda wa Asia hasa nchi za Malaysia, India, China, Japan, Korea nk ili wawaalike wawekezaji waje kujadili fursa zilizopo na wapi wanaweza kuwekeza pia wanaweza kushirikiana na watanzania, kongamano hilo linaweza kueleza kiasi cha ardhi ya uwekezaji kilichopo na kuainisha maeneo hayo, miundombinu iliyopo kama umeme, barabara na bandari, sekta binafsi pia ishiri.
Kwa leo naomba niishie hapo DBC