Nyamtalakyono
JF-Expert Member
- Dec 17, 2015
- 795
- 479
Ndugu zangu watumishi wa Mungu nawasalimu kwa jina la Yesu. Napenda kuchukua fursa hii kutoa ushauri kidogo juu ya huduma mnayoitoa.
Mimi si mtaalam sana wa kupangilia mambo lakini najua kwa vile nyie Mungu amewabariki najua mtanielewa. Mara nyingi nimekuwa nikiwafuatilia katika mahubiri yenu kupitia vyombo mbalimbali na kubaini kuwa Mahubiri yenu yamejikita sana kwenye mafanikio, kubarikiwa na hali ya Siasa hasa kuwakosoa viongozi.
Lakini pia nikirejea mafundisho ya Yesu ambaye naamini ndiye tunayejifunza kutoka kwake sijapata kuona akifundisha sana juu ya kubarikiwa tu bali namwona Yesu akisisitiza sana juu ya upendo, kusamehe na kubeba msalaba.
Ushauri wangu kwenu mi nadhani mfuate msingi na mahubiri ya Yesu maana mahitaji makubwa ya wanadamu kwa sasa ni uponyaji wa mioyo yao ambayo imejeruhiwa sana na mambo ya dunia hii na sio kubarikiwa mwilini tu. Maana hata ungekuwa una mali kiasi gani kama rohoni hauko salama hutafurahia hata mali ulizonazo.
Mfano kama mtu hana Amani katika ndoa yake hata akiwa na Gari sidhani kama taishi kwa furaha. Lakini niwakumbushe kuwa mambo yote ya Mwilini tutayaacha duniani lakini ya Rohoni tutaenda nayo Mbiguni kwa baba.
Tupunguze shuhuda za kupata magari na majumba ambayo siku ya kufa hatutazikwa nayo na tuwajenge zaidi waumini wetu kutoa shuhuda zaidi namna Mungu alivyowasaidia Rohoni. Ikumbukwe kuwa hao wanaodai mmewaombea wamepata majumba na magari hawana uwezo hata wa kusamehe na inawezekana hata humo ndani ya makanisa yenu hawasalimiani na wengine wametelekeza hata familia zao.