Ushauri kwa Vyama Vya upinzani

msweken

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
441
1,714
Hapa nchini kuna mambo mengi sana ya kuyajadili na kuyasimamia badala yake upinzani na Watanzania wengi kuijumla wamejikita na Mh. Paulo, ni kweli kuwa mkuu ana mapungufu yake mengi sana na amefanya mambo mengi sana yanayo wakera wengi ila pamoja na hayo yeye hapaswi kuwa Agenda kuu ya upinzani, Watanzania tuna matatizo mengi sana ambayo tulitegemea upinzani ndiyo mngeyawekea kipaumbele. Kuyataja tu kwa ufupi

1. Changamoto ya ajira kwa wahitimu

2. Changamoto ya mikopo kwa wanafunzi

3. Kutokulipwa stahiki kwa wafanyakazi

4. Ongezeko la makato ya bodi ya mikopo

5. Kutokulipwa mafao ya wastaafu

6. Kukosekana kwa madawa hospitalini

Haya ni machache katika matatizo mengi yanayotukabili watanzania, haya ndiyo yanayomuathiri yule Mtanzania wa kule Sumbawanga, Lindi, Mtwara, Tabora na Tanzania nzima kwa ujumla. Hivi mnadhani Watanzania tutawakumbuka kwa kumtoa Paulo madarakani? Tutawakumbuka kama mtailazimisha serikali itoe ajira kwa wahitimu wetu, tutawakumbuka kama mtailazimisha serikali iwalipe stahiki zao wafanyakazi, tutawakumbuka kama mtailazimisha serikali ipeleke madawa ya kutosha mahospitalini na sio kwa kumtoa Paulo Dar na kumrudisha Koromije.

Goli la kutokuhamisha lilipaswa liwe hizo changamoto na sio Paulo, issue ya Paulo ingetakiwa iwe ka agenda kadogo ambacho kasingeamisha misingi ya agenda kubwa ambazo ni changamoto walizonazo Watanzania wengi.

Nakaribisha mapovu maana Nguo nimeziandaa na maji ninayo kasoro sabuni tu.
 
mkuu, nakubaliana na hoja ila huoni hiyo kazi kwa asili inatakiwa kwenye TU au umbrella yao?
Fikiria mpaka sasa pamoja na masaibu yote hayo TUCTA japo watu kisheria lazima waichangie lakini haijaonesha nia ya kutetea wanachama wake
Kama baba huwezi kulisha family unategemea baba wa jirani akusaidie this is bullshit
 
Back
Top Bottom