Ushauri kwa viongozi wa Vyama vya Siasa vya Upinzani

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,227
6,670
Naamini, tangu Serikali ya Awamu ya Tano, ikiongozwa na Rais Magufuli, ianze kazi hadi sasa kuna mengi ya kujifunza.

Kubwa zaidi ni agenda zilizokuwa zinapamba, kupandisha sifa na umaarufu wa viongizi wa vyama vya siasa.

Wakati agenda hizo ziliishia kwenye mikutano ya hadhara na vyombo vya habari, serikali inatekeleza kwa vitendo.

La ajabu, viongozi wa vyama vya upinzani vinabeza juhudi hizo, tena kwa maneno kwenye vyombo vya habari, badala ya kutekeleza kwa vitendo, kwenye maeneo waliopata ushindi.

Ili kuweka ushindani wenye tija, upinzani uoneshe kwa vitendo nia yao dhabiti ya kuleta mabadiliko kwenye jamii.

Tumechoka na ahadi.
 
Magufuli akiangalia kioo anajiona kafanana na Kagame na Museveni nauhakika hatong'oka huyu hata baada ya miaka 10 yake kumaliza.
 
Back
Top Bottom