Ni vigumu sana kutenganisha dini na siasa kwani dini ina nafasi kubwa sana kupata siasa safi. Kitu cha msingi ni kutotumia dini vibaya kutaka kujinufaisha kisiasa ikiwa ni pamoja na kupotosha tafsiri ya nukuu zinazonukuliwa. Tukiwa na viongozi wa siasa aambao ni waadilifu kwenye dini zao hapo tutakuwa na uhakika wa kupata siasa safi isyo na fitina na mchezo mchafu.
Ushauri huu hautaungwa mkono, niambie Padri slaa, mchungaji msingwa, mchungaji natse watumie maneno gani kushawishi umma wanapukuwa kwenye mikutano ya hadhara?
Usisahau kwamba ushawishi wako wa kisiasa ulitokana na kuwachanganya waumini wao. Watu wengi ikiwemo wapiga kura wa viongozi hawa wa kidini/kisiasa bado wanawatambua hawa kama watu "anaopata maono kutoka mbinguni" hivyo huwa hawapingwi.
Nimehudhuria mikutano mingi ya CDM; ambapo kumekua na baadhi ya vitu vyenye kuhitaji marekebisho "kidogo" . Kila mmoja anayo style yake ya kukamata saikologia ya hadhara. Ila kumekua na tabia "mbaya" ya kusisitiza jambo kwa kwa kutumia vifungu vya maandiko Matakatifu:.......kwangu mimi naona ni Vibaya "Mno" ; hasa ukizingatia kipindi hiki ambapo nchi imekua delicate na maswala ya kidini. unaweza kusikia kiongozi anaapa akisema....
"hata kur_an inasema"
......"hata Biblia inasema"
....."kwa wale wanaosoma Biblia"
...etc.
Na utagundua tu kwamba sio vizuri maana ikitamkwa tu hivi, basi uma una sisimuka kidogo na kutizamana nyusoni.
CDM ndio chama pekeyake cha kuibadili hii "kwasasa" .
Dalili za kidini aachiwe JK na LIPUMBA(kama alivyokiri mwenyewe)
_-_-_-JICHO LA BUNDI_-_--_