Me huo mstari wa mwisho tu ndugu yangu " kwa wale ambao mmashachelewa poleni, Ila jitahidini".
Ndugu kuna kikomo cha kuolewa? Na je wajitahidi kufanyaje, kulazimisha ndoa au?
Karibu Kila msichana anatamani kuolewa na kuwa na familia yake as long as amempata mtu sahihi kwake na anajiona yupo tayari kwa ndoa . Kama mtu sahihi hajapatikana, ulazimishe kuolewa kwa sababu ni heshima au kwa sababu umri unakwenda au kwa sababu wazazi na jamii inakupa pressure?
Ni bora ukachelewa kuolewa, lakini ukaolewa na mtu sahihi. Kuliko kuwahi kwa sababu ya hizo pressure afu ukajikuta unajutia maisha yako. Ikitokea umepata mtu sahihi na ukaolewa mapema, hongera zako. Wale ambao watachelewa kuolewa kwa sababu zao pia, basi maamuzi yao yaheshimiwe.