Ushauri kwa Tundu Lissu juu ya Makontena ya ACACIA

TangataUnyakeWasu

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
1,268
1,587
*Ushauri kwa _Tundu Lisu_*

Ukiwa Kama mwanasheria mashuhuri nakuomba ulisaidie Taifa na hawa mapepari na majizi ya rasilimali zetu wanaojiandaa kwenda kulishitaki Taifa letu kwenye Mahakama za kimataifa kisa tu Taifa limechukua hatua kwa namna tunavyoibiwa rasilimali zetu na hao mapepari wanatumia mgongo wa sheria tena walizotunga wao na zinabeba hao hao kuendelea kutunyonya kwa kigezo cha Mahakama za kimataifa.

Ni kweli kutokana na sheria za kimataifa zilivyokaa ikitokea ACACIA wakaenda mahakamani Taifa litawalipa fidia kubwa sana, pesa ambazo ni kodi za sisi wananchi wa hali za chini. Ifahamike kuwa hawa wawekezaji wanatuibua kwa kutorosha rasilimali zetu wakijua mwisho wa siku kuna sheria za kimataifa zilizotungwa na hao hao zitawatetea tena. Kwa lengo la kizalendo nakuomba Tundu Lisu Ukiwa Kama Rais wa TLS na pia Mtanzania mwenzetu andaa timu yako ya wanasheria mahili (Akina Malya, Mabere Malando, Chenge) na wengine wengi kuhakikisha mnaenda kupambana nao huko kwenye Mahakama zao wanakopanga kwenda kulishitaki Taifa.

Kwa hili la rasilimali zetu tuweke uvyama pembeni tuungane kumuunga mkono Mh Raisi kwa hatua alizochukua. Ni kweli kabisa bado Kuna changamoto nyingi kwenye uwekezani wa rasilimali zetu haswa katika upande wa mikataba na sheria mbovu zinazosimamia hiyo mikataba iliyosainiwa na viongozi wetu ambao pia ni Watanzania wenzetu (wengine bado wapo madarakani eg. Akina Chenge kipindi hicho akiwa mwanasheria mkuu wa Serikali) .

Hivyo basi kwa hatua za awali hawa wanaojiita wawekezaji tukiwashinda kwa hili la mchanga hayo mengine ya mikataba kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu siku moja pia tutayafikia tu.

*UKWELI HUWA UNA ASILI YA KUUMIZA, ILA KWA HILI LA RASILIMALI ZETU TUSIMAME UPANDE WA UKWELI*
 
images(1).jpg

Ndio hivyo.
 
Hivi mbona mnamuandama Lisu ?! Mwambieni mwenyekiti wenu amualike si kujipereka kwa wenye nyodo kina Masaju. Huwezi kufanya kazi ambayo hukukabidhiwa official.
Mkuu mm nimetoka tu ushauri na siyo kumwandana.

In short mm siyo kijana wa Lumumba Fc
 
Ushauri wapewe mara ngapi mkuu? Au wewe umashuka leo duniani kutoka mwezini?

By the way, our presido has guts!
 
Acha vitisho vya kulipa.Nchi hata isipolipa hakuna kitakachotokea.Kampuno inaiba waziwazi halafu iacjwe eti kwa sababu ya mkataba.Mkataba naPublic interest kipi kiko juu.Uwekezaji ktk nchi hii haujadhibitiwa vizuri.Ni wizi mtupu. Nyerere alishasema madino haya tuyaache.Lakini baada ya kifo chake Mkapa akafungua milango ya uwekezaji kwenye madini kiholela na bila kuongozwa na uzalendo.Haya ndo matokeo yake.Mkapa ktk hili anawajibika.
 
Mkuu mm sitoi vitisho bali nimetoa tu ushauri Kama mwananchi wa kawaida.

Kuhusu kuwalipa hilo liko wazi endapo watatupeleka Front na kutushinda Kesi.
 
Lissu mwenyewe hazijui contents zilizoko kwenye hiyo mikataba! Ndiyo maana alikuwa akipiga kelele kuwa iwekwe wazi! Sasa kama mtu anawashwa ni wajibu wake kuonyesha panapowasha ili wenye kucha wamkune, vinginevyo mnamwonea Lissu
 
Acha vitisho vya kulipa.Nchi hata isipolipa hakuna kitakachotokea.Kampuno inaiba waziwazi halafu iacjwe eti kwa sababu ya mkataba.Mkataba naPublic interest kipi kiko juu.Uwekezaji ktk nchi hii haujadhibitiwa vizuri.Ni wizi mtupu. Nyerere alishasema madino haya tuyaache.Lakini baada ya kifo chake Mkapa akafungua milango ya uwekezaji kwenye madini kiholela na bila kuongozwa na uzalendo.Haya ndo matokeo yake.Mkapa ktk hili anawajibika.
Tunailipa Dowans kwa kosa letu la kukataa kuibiwa,Tunawalipa wachina wa samaki! Kwa kosa hilohilo! The next is? ACaCiA? Tuwe macho
 
Back
Top Bottom