Ushauri kwa TAMISEMI kuhusu ajira za walimu

Kkimondoa

JF-Expert Member
May 31, 2014
4,453
4,933
Naomba nichukue fursa hii kuishauri TAMISEMI kuhusu ajira za walimu inazo tarajia kuzitoa ,ni kwamba
Kama inawezekana wapangieni walimu shule moja kwa moja kutoka huko huko maana hii ya kuwaachia maafisa elimu wilaya ina changia sana mazingira kupanga vituo vya kazi kwa rushwa na kujuana

Ndio maana kumekuwa na walimu wengi sana shule za mijin wakati vijijini walimu ni wachache sana na walimu wengi hupangwa mijin kutokana na labda rushwa au kujuana

Ushauri . kama kuna uwezekano ni bora TAMISEMI mkapanga shule hukohuko moja kwa moja ili kupunguza walimu wengi kujazana shule za mijin hasa wale wenye kipato na kujuana na wale watoto wa masikini ndio hasa wanaotupwa maporini

Unakuta shule moja mjin inawalimu hadi 7 wa physics au hesabu halafu vijijini shule hazina hata mwalimu mmoja wa physics au hesabu hili ni tatizo

Niwapongeze kwa mwaka jana mlijitahidi kiwapangia walimu wa sayansi moja kwa moja,kwa kiasi fulani ilisaidia kuziba mapengo lakini nashauri fanyeni hivyo kwa masomo yote sababu swala la uhaba wa walimu hasa kwa shule za vijijin upo hata kwa walimu wa masomo ya art unakuta shule nzima kuna mwalimu mmoja wa geography au kiingereza hilo ni tatizo.

Lakini pia baadhi ya maofisa elimu wasio waaminifu hutumia fursa hiyo kupata rushwa ya ngono kutoka kwa walimu wa kike ili wawapangie shule za mijini kitu ambacho pia kimekuwa si tatizo kwa walimu wa kike kukifanya na wakapangiwa shule nzuri

Tunaomba TAMISEMI ili kupunguza uhaba wa walimu shule za vijijin zingatieni hilo la kupanga shule moja kwa moja angalau laweza kusaidia kidogo.
 
Mkuu kama ni mfuatiliaji mzuri zoezi hili la kuwapangia walimu moja kwa moja shuleni limeanza tangu mwaka jana (ajira zilizopita) kwa walimu wa sayansi.
isipokua walimu wa sanaa na biashara ndio hupangiwa halmashauri, so I hope even this time wataendelea na utaratibu wao
 
Back
Top Bottom