Ushauri kwa Shirika la Nyumba la Taifa

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
13,095
22,705
Habarini wadau:

katika maisha ya mwanainchi wa kawaida kuna mahitaji muhimu ili maisha yaweze kwenda na maendeleo yawepo. Kwanza ni chakula kwa maana ya lishe kamili na ushauri bora wa matumizi ya chakula mbadala wa dawa. Pili, mavazi kwa maana ya nguo, viatu na chochote kivaliwacho na mwili ili kumpa mtu heshima ya kujisitiri mbele ya jamii inayomzunguka maana mavazi ni sehemu ya heshima kwa mtu yeyote.Tatu, ni maladhi au makazi kwa kiswahili cha sasa kwa maana sehemu ambapo mtu atapaita nyumbani kwake na akiwapo hapo anaweza hata kulegeza mkanda wa suruali yake au akakaa na boxer bila hofu ya kubugudhiwa na mtu.N'ne ni hitaji la elimu au taarifa kwa maana binadamu anahaki ya kupata taarifa juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea katika mazingira anapoishi kupitia vyombo vya habari, social networks, internet, lakini pia elimu ya darasani ya kawaida hii tunayoisoma.

Nimeamua kuyataja mahitaji yote ili hata wasioyajua wayajue ila ajenda kuu ni kuhusu hitaji la maladhi ama makazi. Kiujumla katika hali ya kawaida ingependeza idadi ya watu iendane sawa na uwezo wa serikali wa kuwapatia mfumo rasmi wa makazi kwa maana ya majengo ambayo yapo tayari na yanasubiria wamiliki waje kuyatwaa kutoka serikalini na kuanza kuishi ndani yake kwa utaratibu maalumu wa kuyapata na kumilikishwa.

Kwa hapa nchini kwetu na nchi nyingi ambazo zipo katika uchumi wa kujikongoja, swala la makazi hubakia kuwa ni jukumu la raia mwenyewe binafsi bila serikali kutia mkono hata kidogo au kumpa sapoti. Nadhani wengi wenu tayari m'meshakutana na hii kadhia ya kupata makazi rasmi ya kudumu na yenye hadhi nzuri kwa maana yenye kujitoshereleza kwa nafasi, miundo mbinu ya barabara nzuri za mitaa iliyonyooka, anuani ya posta, mifumo ya gesi ya kutumia nyumbani, maji, na umeme. Kiwango kikubwa cha wananchi wanajenga nyumba za kuishi bila hata ya uelewa wa mamlaka za serikali ambazo zinawajibika au zinajukumu la kuhakikisha raia wa nchi hii anapata sehemu salama ya kuishi bila kukiuka taratibu za kiusalama kama kujenga karibia na viwanda, kando ya uwanja wa ndege, chini au kando ya nguzo za umeme, au mabondeni na karibia na njia kuu za maji kuelekea baharini.
Raia anawajibika kujitafutia kiwanja tena kwa gharama kubwa sana ambayo haistahili na ni kosa kisheria kwa maaana ardhi ni mali ya uma na hivyo basi dhamana ya usimamizi ipo serikalini na haitakiwi mtu baki kuiuza kwa bei ya kibiashara kwa maana ni haki ya kila mtanzania kuweza kumiliki sehemu ya makazi yake, kutafuta wataalamu wa kupima kwa gharama zake mwenyewe, Kuanza ujenzi wa nyumba bila suppport yoyote na hatimaye ujenzi kuishana mtu kuwa na makazi yake ya kudumu na familia yake. Hii kwa watu wengine inaweza kuonekana ni kitu cha kawaida ama si tatizo kwa maana ni mfumo ambao tumeukuta kwa wazazi na pengine na sisi hatua za haraka zisipochukuliwa utaendelea kuwepo hadi kwa wajukuu zetu siku zijazo.

Kiukweli huu si mfumo mzuri kwa raia wa nchi tajiri kama tanzania katika kujipatia makazi ya kuishi kwa maana ni wa gharama ya juu sana kwa mtanzania wa hali ya kawaida kumudu ukizingatia kipato cha mtanzania wa kawaida huwa si cha uhakika maana wengi wao hawana ajira rasmi na wengiwao ni vibarua tu katika shughuli za watu na kipato chao hakiwaruhusu hata kuweka akiba. Hebu jaribu kutafakari process ya kutafuta kiwanja, kukilipia,kukipima, kukipatia hati, kuanza ujenzi, hadi nyumba inakamilika huwa inakuwa ni kiasi gani?!

Nimejaribu kuwaza nikaona nilete hapa huu mjadala ili mimi na wewe tuwashauri shirika la nyumba la taifa kwa niaba ya serikali kutia maoni yetu hata kama hawataona au wataona na hawatatilia maanani maoni yetu, mimi na wewe kama raia tuwe tumeshatimiza wajibu wetu wa kikatiba na kiraia wa kujadili na kutoa maazimio ya kimaendeleo ya jamii yetu.
Mimi nashauri kwamba hivi ni kwanini swala la kuhamisha wakazi katika maeneo yasiyo rasmi kwaajiri ya makazi ya binadamu kama mabondeni, kandoni mwa barabara, au maeneo yenye msongamano na ujenzi usio wa ramani za kueleweka kama vingunguti, mburahati, temeke, baadhi ya maeneo ya ilala, tabata kimanga na segerea, kinyerezi, yote haya yakiwa yamejengwa kiholela bila utaratibu maalumu wa mpangilio wa ujenzi na kuacha nafasi ya hewa na njia za kupita watu na vyombo vya usafiri.

Nadhani serikali kupitia shirika la nyumba la taifa lingeyatambua haya maeneo kuwa si rasmi kwaajiri ya makazi ya watu na lingeanza program maalumu ya kuhamisha kaya moja moja yaani nyumba au familia moja moja na kuzialocate sehemu nhingine ikiwa ni zoezi ama program endelevu. Nasema hivi kwasababu serikali yetu haina uwezo wa kuwaamisha wakazi wengi kwa wakati m'moja kwasababu hii huwa ni gharama na kuna watendaji wa hizo operation huwa wanaleta ubashite na ushenzi wa kufanya ubadhilifu kwa kudhulumu waathirka ama kudanganya data serikalini, lakini kubwa zaidi kuwahamisha watu wengi kwa wakati m'moja ni gharama sana maana itahusisha kuwalipa fidia au kuwapatia makazi mapya kwa wakati moja. Ila kama serikali itaweka hili kama zoezi la kudumu basi hata ikiamua kudeal na mtu nyumba kumi kumi na kwenda hatua moja hadi nyingine na kuhakikisha watokomeza nyumba zotw katika maeneo haya na hizi familia zimepata makazi mapya salama na yaliyo katika mpangilio wa kisasa wa kitaalamu chini ya mipango miji then tanzania itavunja rekodi afrika nzima katika program ya kisasa ya kubadili mpangilio wa miji kutoka kuwa na makazi ya hovyo hovyo kama ya sasa na kwenda makazi mapya ya kisasa kama ulaya.
Kama serikali watatumia mfumo huu itasaidia kupunguza gharama maana kuziallocate kaya kumi kila baada ya muda fulani itasaidia kufanya tathimini sahihi na kuweza kuwapatia makazi mapya bila kuharibu utaratibu na hii itafanya serikali kupata matokeo sahihi ya kubadili makazi kutoka holela kuwa rasmi. Hebu wazia eneo kama mburahati kila baada ya muda fulani kuna nyumba kumi zinavunjwa na kunabakia kweupe hakuna nyumba mpya inajengwa maeneo hayo, kisha baada ya muda eneo linabakia kuwa jeupe kama hakukuwahi kuwepo nyumba na serikali inaanza kupangilia upya utaratibu na miundo mbinu katika hilo eneo. Hili zoezi likiwa ni endelevu mikoa yote kwa muda wa miaka kadhaa tutaanza kujionea mpangilio mzuri sana wa makazi na miji na itasaidia sana serikali kufanya shughuli zake za kimaendeleo.

Ni haya tu kwa leo wadau naomba tuchangie mawazo tujue nini tunafanya. Maana hata mheshimiwa raisi wetu mpendwa dk. John Pombe Magufuri ameshaweka wazi kuwa kupiga kazi tu kuanaanza na kauli zetu, tuache kulalamika tushow support hata kwa maoni ili tusiwe sehemu ya walalamishi ambao hata ukiitwa ukaulizwa ni nini ulishawahi kusema au kuchangia maoni hakikusikilizwa unakosa ushahidi.
 
Kule shuleni kuna kitu wanafundisha kinaitwa "Executive Summary" ni muhimu sana ili kuleta hamasa ya kusoma ngwini ndefu kama hii.
 
Kule shuleni kuna kitu wanafundisha kinaitwa "Executive Summary" ni muhimu sana ili kuleta hamasa ya kusoma ngwini ndefu kama hii.
 
inatege
Kule shuleni kuna kitu wanafundisha kinaitwa "Executive Summary" ni muhimu sana ili kuleta hamasa ya kusoma ngwini ndefu kama hii.
Inategemea na malengo ya unachoandika......mimi hapa sijaandika business plan au prospectus ila nimeandika article fupi ambayo si rasmi so sipo chini ya kanuni za uandishi rasmi na nimeandika kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa wadau sasa ukiona umeona kazi kuisoma jua haijakupa interest pengine wewe ni unapenda kusoma udaku kuliko mijadala ya maendeleo na ndio maana hii kwako imekuwa kazi kusoma au kukusisimua. But thanks kwa ushauri next time nitapunguza maneno ili watu wa jamii yako waweze kusoma.
 
Back
Top Bottom