Ushauri kwa IGP - Polisi waongeze umakini

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,071
Nampongeza IGP na jeshi la polisi kwa ujumla kwa kuona umuhimu wa kuimarisha ulinzi kwenye vituo vyetu. pamoja na kuimarishwa huko kwa kuongeza idadi ya askari walinzi wa vituo, kuweka askari wenye silaha, na kuweka standby bodaboda lakini bado kuna changamoto chache ambazo mkuu unapaswa kuzielewa.
  1. Askari kuendelea kuishi kwa mazoea ya kawaida
    • Kama ukiwa makini unaweza kuona kuwa bado kuna baadhi ya askari wanafanya mazoea mabaya kama watumishi wengine wa umma wa Tanzania. pamoja na kuwa kwenye state of high alert bado kuna askari wenye silaha unawakuta wanashughulika na kusoma magazeti, wanashughulishwa na simu zao au wapo wanapiga soga either wao kwa wao au na watu wengine waliovaa kiraia. nadhani kwenye state ya sasa, ni risk kwa askari mlinzi akiwa kazini kuwa na multiple tasks maana itampunguzia umakini.
  2. Uwepo shughuli nyingine za kijamii zisizo rasmi kwenye vituo
    • Pamoja na kuweka vizuizi kwenye maeneo ya vituo vya polisi ili kutoruhusu watu wasikatize, lakini bado kwenye vituo vingi vya polisi kuna shughuli nyingi zinazozua mikusanyiko isiyo rasmi ambayo pia inatoa access kwa watu wasiokuwa askari kufika karibu na ofisi. watu wa breakdowns wamewekeza kwenye vituo na wanashinda hapo, lakini pia wapo baadhi ya wafanyabiashara wa vyakula, magazeti na bidhaa nyingine au huduma nyingine ndogondogo wanakuwa maeneo karibu sana na vituo, angalau kwa sasa, wasitishe huduma hadi hapo hali ikiwa shwali.
  3. Mlundikano wa magari na bodaboda
    • mkusanyiko mkubwa wa magari na bodaboda zilizofikishwa vituoni kutokana na matukio mbalimbali vinawaweka polisi kwenye wakati mgumu wa ku-manage eneo lenu, hata likitokea tatizo (ambush) hata nyinyi wenyewe mnalazimishwa ku-escape kupitia maeneo machache sana.
  4. Askari wa usalama barabarani kutoshiriki operation
    • siwezi kusema najua ni kwa jinsi gani askari wetu wamejipanga, ila kwa sasa, hawa askari wa barabarani wanapaswa nao waache kuabudu kuandika fine tu, nao check point zao zingejita Zaidi kwenye kuchunguza watu tunaokuwa ndani ya magari kuliko kulitazama gari/bodaboda. waharifu wangeogopa Zaidi kama wangejua kuwa sasa hata wao watahojiwa wakiwa kwenye vyombo vyao.
  5. ubabe dhidi ya wananchi
    • mnahitaji sana support ya raia so tushirikiane badala ya kufanya ubabe
ushauri
Boresha ulinzi na rekebisha mpasuko unaoendelea baina ya wananchi na jeshi lako.
 
Nice write up

Nikiongezea msisitizo

Askari washirikiane na wananchi. Waache kujitweza na kujiona wao si sehemu ya jamii

Together we are strong, devided we fall
 
Wapelekee central pale maoni yako,sidhani kama hata anasomaga jf huyo jamaa yako.
 
Mkuu umerusha jiwe Kwenye Giza utasikia yowe muda si mrefu.
Hapo utajua ujumbe ushafika kwa muhusika.
 
Nice write up

Nikiongezea msisitizo

Askari washirikiane na wananchi. Waache kujitweza na kujiona wao si sehemu ya jamii

Together we are strong, devided we fall
Lile suala la polisi jamii walilisimamisha Lakini sidhani kama kulikuwa na scientific evidence juu ya madhara ya Ile operation. Nadhani Kuna vitu vilihitaji kurekebishwa na sio kufuta!
Kwa haraka haraka natamani tungepitia kesi na aina ya uharifu wakati wa mahita, said mwema na wakati huu wa Mangu, kwa maoni yangu wakati wa saidi mwema Hali haikuwa mbaya kama wakati wa mahita! Ila kwa trend inavyoenda Naona kipindi hiki cha mangu nacho kinaweza kuwa kibaya na the only difference kwenye vipindi hivi vitatu ni uwepo or abscence ya polisi jamii! Anyway hizi ni fikra zangu zaidi I hope polisi wamefanyia utafiti na watalifanyia kazi zaidi suala Hili!
Kwangu niliwaona hawa polisi jamii ni kama informers tu, na kwa kuwa wao waliishi nasi muda wote na karibu wote walikuwa ni wenyeji hasa hasa wa maeneo husika, kwao ilikuwa rahisi hata kubashiri tu kuwa huu uharifu anaweza kuwa kaufanya nani, hata kama hakuna leakage wao waliweza kutoa leads kwa wanausalama pa kuanzia na uchunguzi!
Lakini pia, idadi ya polisi haitoshi kabisa, sasa ni kwa jinsi gani polisi wanaziba Hili gap la idadi ndogo?
Uwepo wa mgambo na askari binafsi Kuna ongeza tija kwa kiasi fulani lkn hawa huwa hawaongezi Ile nguvu ya jeshi letu muda wote kwa kuwa wao wanatumiwa na ofisi tofauti! Idara nyingine kama afya, elimu na kilimo zimehusisha makundi ya jamii kwenye utoaji wa huduma au zimeweka kada za chini zenye watu wenye qualifications za chini ambao wanatoa support kwa jamii! Polisi jamii au kitu chenye mfano sawa na huo kinahitajika ktk kuboresha utoaji wa huduma kwa sasa, kwani miji imetanuka. Vijiji vimekuwa na watu wameongezeka mno kufanya wanaohitaji huduma ya polisi kuwa Wengi na kwenye eneo kubwa zaidi ya Ile standard coverage ya vituo vyetu na uwezo wake! Mfano tu kwa eneo la mkuranga ukitoka vikindu Hadi mkuranga Nadhani hakuna kituo kingine cha polisi, stakishari Hadi kisarawe, boko Hadi bagamoyo, mbezi kwa yusuf Hadi kibaha na kigamboni Hadi pemba mnazi! Hayo ni kwa jiji la Dar na Maeneo yake ya jirani! Then how do we support ulinzi?
Vikosi vya jiji vingeundwa na polisi wangeshirikiana na halmashauri zetu, polisi iandae mafunzo kwa polisi jamii watakaoletwa na serikali za mitaa wewe kama sehemu rasmi sasa ya ulinzi shirikishi na wale askari wa jiji au miji waache kujimbizana na wamachinga au mama lishe instead wawekeze kwenye ulinzi wa jiji/miji yao!
 
Polisi waache kufunga vituo saa 12.Kituo cha polisi kinafungwa mageti saa 12!na raia wafunge nyumba zao saa ngapi.
Kitendo cha polisi kufunga milango saa 12,kinaonesha udhaifu mkubwa kinafanya polisi waonekane wanaogopa wahalifu.
Waacheni waingie,lakini muhakikishe wanatoka maiti,
Zamani kulikuwa na msemo"fulani anapaogopa kwangu kama kituo cha polis"maana yake ni kuwa polisi palikuwa sio pa mchezo mchezo kabisa
 
Polisi waache kufunga vituo saa 12.Kituo cha polisi kinafungwa mageti saa 12!na raia wafunge nyumba zao saa ngapi.
Kitendo cha polisi kufunga milango saa 12,kinaonesha udhaifu mkubwa kinafanya polisi waonekane wanaogopa wahalifu.
Waacheni waingie,lakini muhakikishe wanatoka maiti,
Zamani kulikuwa na msemo"fulani anapaogopa kwangu kama kituo cha polis"maana yake ni kuwa polisi palikuwa sio pa mchezo mchezo kabisa
Hapa issue siyo kuogopwa, kinachotakiwa ni ufanisi kuboresha usalama huku jamii yote ikiiona polisi kama taasisi muhimu inayowahudumia.

Msome mleta mada taratibu utamuelewa
 
Back
Top Bottom