Ushauri: Kujitoa NSSF

dontgiveup

Member
Joined
Nov 10, 2014
Posts
22
Reaction score
5
Habari wana jf, kwanza naomba mnikaribishe kwani ni mara yangu ya kwanza kuwa hapa jinsia yangu ni she, niende moja kwa moja kwenye point. Mimi pamoja na wenzangu takribani 40 hivi tulikuwa ni waajiriwa wa kampuni fulani hapa Mtwara kwa muda wa miaka mitatu sasa, mwezi wa, nane mwaka huu tumemaliza mkataba na mwajiri ameshatupatia barua ya kueleza kwamba mkataba umeisha na wengi wetu tumebahatika kupata kazi kwenye kampuni nyingine. Tukaanza taratibu za kuchukua ela zetu NSSF, lakini cha kushangaza hawa jamaa wamegoma kutoa ela kwa madai kuwa taarifa zetu wanazo kwamba tumepata kazi katika kampuni nyingine. Na wakati haya yakiendelea sisi wafanyakazi tulishajiunga na mfuko mwingine wa jamii tofauti na NSSF kwani hatufurahishwi kabisa na huduma zao kwa hapa Mtwara. Leo tumeenda tena kuwauliza kwa nini wanang'ang'ania kukaa na ela zetu wakati barua za kuonyesha kuwa mkataba umeisha tumewaonyesha pia tumeshafanya maamuzi ya kujiunga na mfuko mwingine, jibu walilotoa ni kwamba hata kama michango yetu itapelekwa mfuko mwingine bado hataweza kutupatia ela yetu na kama tunaweza tukashitaki popote. Sasa jamani je hiki kitu wanachotufanyia NSSF ni sawa? Mnisamehe kwa maandishi mengi
 
Sheria inawalinda ni kweli ukishaanza kuchangia Mfuko mmoja hurusiwi kubadilisha na mwajiri atayembadilisha mtumishi Mfuko huku akijua kuwa mtumishi huyo alikuwa ameajiriwa sehemu nyingine na alikuwa anachangia fine yake ni Mil 10 cha kufanya we dai madai yako ofisi nyingine ya NSSF hata Mkoa mwingine kabisa but usiseme kwamba umepata Kazi sehemu nyingine we sema mkataba umeisha na sasa unafanya Biashara zako binafsi hapo utalipwa faster.
 

Hivi mkuu huwa wanalipa akiba yako yote au ni % fulan?
 
Cheki calculation kwenye web yao na unaweza kutumia benefit calculator ipo vilevile kwenye web ukajua kabisa utalipwa sh ngapi
 
Nashukuru mkuu Mwashilungu acha nifanye kama ulivyonishauri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…