Ushauri kuhusu kurudia elimu ya sekondari

Man Ngosha

JF-Expert Member
May 2, 2012
219
69
Habari zenu wadau,
Nina mdogo wangu ambaye alihitimu kidato cha nne mwaka 2011 na hakupata matokeo mazuri,alishauriwa kurudia masomo yake lakini haikuwezekana kutokana na sababu mbalimbali.Napenda kujua/kupata ushauri wa mambo yafuatayo:-

1. Kwa sasa,anaweza kuruhusiwa kurudia kidato cha tatu yaani form three ili aje afanye mtihani wa kidato cha nne?

2. Kama hilo hapo juu linakubalika, nini cha kufanya?

3. Kama 1 na 2 hapo juu hayawezekani, nini cha kufanya ili kijana huyu aweze kufanya tena mtihani wa kidato cha nne na hatimaye kupata alama za kumuwezesha kuendelea na masomo mengine ya ngazo zinazofuata?

Natanguliza shukurani.
 
Asubiri mwakani Sasa Muda wa kujiandikisha ushafungwa

Na ajiandikishe kurudia masomo aliyofeli tu
 
Labda kama alipata mzinga vinginevyo anaweza itafuta degree kupitia certificate, diploma, then ...
 
Yan elimu saiv inazid kuwa nguo wanafunzi inabidi wakaze.atafute credits kisha aende shule akasome kwa bidii
 
Alipata alama "D" tatu tu katika masomo yote aliyofanyia mtihani,sasa tulifikiri angepata nafasi kwa vyuo vya afya kwa ngazi ya Basic Technician, lkn huko nako wanahitaji awe na "D" nne. Hapo ndo limeanzia wazo la yeye kurudia mtihani mtihani wa kidato cha nne au kurudia masomo aliyofeli.
 
Pia inaruhusiwa kusoma private school kwa shart lakuanza Form3 kwa mujib wa necta kam ataweza mpeleke,,, au aka risit paper kwamasomo alofeli pia inaruhusiwa
 
Failed ni yule aliyepiga zero yaani four ya 34 ambayo ni D moja tu au kupata f masomo yote na ndio maana hawapewi cheti, ila kama ulipata cheti chochote cha necta unaweza kusoma chuo hadi ukamaliza elimu ya juu ila kuanzia certificate.
 
Failed ni yule aliyepiga zero yaani four ya 24 ambayo ni D moja tu au kupata f masomo yote na ndio maana hawapewi cheti, ila kama ulipata cheti chochote cha necta unaweza kusoma chuo hadi ukamaliza elimu ya juu ila kuanzia certificate.
Duuuh kuna four ya 24
 
Pia inaruhusiwa kusoma private school kwa shart lakuanza Form3 kwa mujib wa necta kam ataweza mpeleke,,, au aka risit paper kwamasomo alofeli pia inaruhusiwa
meinkemp hili ni la kweli? ebu tupe reference ya authority. Nina tatizo hilo kwa kijana wangu! This will be great! Please
 
Pia inaruhusiwa kusoma private school kwa shart lakuanza Form3 kwa mujib wa necta kam ataweza mpeleke,,, au aka risit paper kwamasomo alofeli pia inaruhusiwa
Hiyo ya kuanzia form three ipo?manake nimesikia kwamba ni lazima afanye mtihani wa form two ili apate namba then anaendelea,Hapo ndo sijaelewa vyema.
 
basi kurisit kwa mwaka huu amechelewa ila kama uko dar mpele pale MAPAMBANO TUITION CENTRE MWENGE NYUMA YA NAKIETE PHAMACY ataanzia 4m3 na mwakan atajisajiri kwa namba yake ile ile ya 4m4 uku akisoma masomo ya 4m4 na atafanya mtiani kama private candidate yaan PC wako vizuri kwa ushauri zaid fika hapo ofisin kwao mwenge shuka itv
 
Back
Top Bottom