USHAURI.. Je naweza kufuga kuku wa kienyeji ndani nkawahudumia wakiwa ndani?

kijana255

JF-Expert Member
Mar 5, 2017
216
250
Habari wakuu kama mnavyojua mambo ya ajira ni pata potea, nataka nianzishe kimradi changu cha kuku ila wa kienyeji, ss sina sehem ila kuna chumba cha nje kipo wazi..swali ni je kuku wa kienyeji wanaweza kaa ndani ushauri kwa wataalam natanguliza shukrani...
 

Vitalis Msungwite

Verified Member
May 11, 2014
2,086
2,000
Labda uanze nao wakiwa wadogo, wakubwa waliozoea kutembea tembea utawapa stress sana na huenda wasikue vizuri au wakaacha hata kutaga.
 

luhuye

JF-Expert Member
Mar 20, 2017
294
250
inawezekana ila ujitaidi kuwaletea majani ukizembea mayai yatafanana na yale ya kisasa pia hicho chumba kiwe na hewa ya kutosha
 

Zamaulid

JF-Expert Member
May 25, 2009
17,800
2,000
Anza na wenye miezi miwili, hao huwa hawahitaji uangalizi mkubwa sana ila kama unatotolesha mayai ya kienyeji kwa mashine na unaweza kuwa na chanzo cha joto unaweza ukaanza na wa umri wowote
Hivi nikiwawekea chanzo cha joto kuwa taa ya bulb...inatakiwa iwe umbali kiasi gani toka kwa kifaranga....inaponing'inia

Sent from my TV
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom