Biashara hii unafanya kulingana na soko + mtaji wako, kama unalenga kuuza kwa jumla lazima uanza na kilo nyingi ambazo sio chini ya kilo 300, inategemea mchele gani unategemea kuuza kama wa kawaida au super, mfano super kwa mbeya ndani ndani huko mashambani kilo ni 700, 800 - 900 ukifika jujuu zaid mpaka mashineni ni 950 -1300, mfano ukapata kwa 900x300 = 270,000 usafiri wako kwenda mbeya na kurudi ni 100,000 kulala, kula na mengneyo kwa siku 3-4 ni 100,000 usafiri wa mchele kutoka shambani mpaka center to dar ni kama 50,000 kutoka unaposhushia (manjese, jangwani, mbezi) mpaka sokoni au dukani kwako ni kama 30,000 kwa haraka haraka ni jumla ya kama 500,000 kwa kilo 300. kwa bei ya jumla utauza 2,000 ili muuzaji wa dukani auze 2,300 kwaiyo 2,000 x 300 = 600,000 (faida 100,000) kwa wiki 3 mpaka mwezi.
Ushahuri: ili ikulipe lazima uchukue ngalau kilo 1,000