Kama ulivyomchukua mwanao mwanzo basi endelea kumtunza bila kuwabughudhi ndugu wa marehemu mzazi mwenzio.
Sioni kama ana haki kubwa unayohisi anaikosa, kama ulivyokosea wewe kumpa haki ya kuishi na mama yake kwenye utoto wake. Wewe ulianza kumnyima mwanao haki yake kubwa na ya msingi, hao ndugu wanamalizia tu.
Tulia ulee mwanao, wao waache na maisha yao...naamini mtoto alimuhitaji zaidi mama kuliko Mali za mama.
Watakuja wanasheria. Ila Kwa hali uliyoelezea ni busara usijishughulishe na Mali za marehemu. Ndugu ndio wataamua. Lea mtoto wako. Pole Kwa changamoto.Nilitaka ushauri wa kisheria na sio hadithi za mtaani zisizo na logic za kisheria, na ndio maana kuna mambo sijataka kwenda deep sana
Kiufupi ni kwamba marehemu alikuja na kumuacha mtoto kwa mama yangu na kutokomea....... nisinge weza kumnyang’anya mtoto ambaye bado alikua ananyonya
Alikuja ku regret baadae sana na mtoto akawa anakwenda likizo kwa mama yake kila mwezi wa 12
Mimi nashauri uwaache hao ndugu wa marehemu waaamue vile wapendavyo kwenye umiliki wa hizo mali. Wala usiingie kwenye mgogoro wa kutaka kuwa msimamizi wa mirathi, na wakati hukuwa mume halali wa marehemu.
Wasimamizi sahihi wa mirathi ni ndugu zake.
Binafsi nakuunga mkono sehemu moja tu ya kukataa kumuacha mtoto wako alelewe kijijini, kisa kuna mali za urithi wa mama yake. All in all, pole sana kwa changamoto uliyopitia.
Nyumba ipo Tanga? Au ipo mkoa mwingine?Mkuu nashukuru kwa ushauri
Ofcoz wasimamizi watakua wao,
Hofu yao kubwa ni kwamba watakapo kwenda mahakamani na kutaja marehemu kaacha mtoto mahakama LAZIMA itaamuru mali ziwe za mtoto chini ya msimamizi wa mirathi, hapo sasa kaka mtu atakosa uhuru wa kuuza nyumba na kiwanja
Ndio maana wanata akae naye yeye mtoto ili ku justify kuuza mali kwa mgongo wa matumiza na ada za mtoto
Maana walisha leta hoja mali ziuzwe zote(hofu yao ni mahakama na sio mimi)
Na mimi sigombanii mali ila napinga kujustfy kwa kumchukua mwanangu waishi nae
Mimi sikujua kabisa kama marehemu ana nyumba na kiwanja hivyo wakati nakwenda huko sikufikiria kabisa mambo ya mali zaidi ya kudhani labda wakifatilia mafao wanaweza kuamua tu kindugu mtoto watampa kidogo..... aikua issue kabisa kichwani mwangu
MSIMAMO WAO NI MTOTO AKAISHI TANGA